Top Leaderboard Advert

ZSSF

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

PBZ_new_logo

Zanzibar Diaspora

Interactive

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, February 11, 2016

Mapato Hospitali ya Muhimbili yaongezeka kwa asilimia 60

By Herieth Makwetta, Mwananchi
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza mapato yake kwa asilimia 60, baada ya kuboresha usimamizi na kupunguza kero za wafanyakazi, huku ikitekeleza kwa asilimia 100 maagizo matatu ya Rais John Magufuli.
Maagizo hayo yalitolewa na Dk Magufuli siku nne baada ya kuapishwa alipotembelea hospitali hiyo, Novemba 9 mwaka jana yametekelezwa kutokana na kuhudumia wagonjwa wengi zaidi na kwa wakati.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya MNH katika siku 100 za Rais Magufuli madarakani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema hospitali hiyo imeongeza uzalishaji wenye tija pamoja na kiwango cha ukusanyaji wa mapato.
Alisema kwa Desemba pekee, walikusanya Sh3.3 bilioni kutoka wastani wa Sh2.7 bilioni ilizokuwa ikikusanya kwa kipindi cha miezi mitano iliyotangulia.
“Tumepiga hatua, kwani Januari mwaka huu tumeweza kukusanya kiasi cha Sh4.3 bilioni. Katika mipango yetu ya muda mfupi iliyopo sasa tumepanga kukusanya Sh6 bilioni ifikapo Julai mwaka huu,” alisema.

Ajali yaua 11 Tanga, yajeruhi 29


By Mwandishi Wetu, Mwananchi Digital
Tanga. Watu 11 wamefariki dunia leo huku wengine 29 wamejeruhiwa baada ya Basi la Simba Mtoto kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Pangamlima wiliyani Muheza.
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa Basi la Simba Mtoto lilikuwa linatokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam.
Kamanda Mihayo ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea mapema leo baada ya dereva wa lori kuhama njia na kukutana uso kwa uso na basi hilo.
Pia kamanda Mihayo amesema kuwa, kati ya watu 11 waliopoteza maisha ni pomoja na madereva wa magari hayo mawili.
Kamanda Mihayo ameongeza kuwa majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Muheza huku jitihada zikifanyika kuwapeleka abiria watano ambao hali zao ni mbaya katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro.

HAYA NI MAKUBWA JAMANI KUTOKA YOU-TUBE!!!


UMESAHAU DOCS ZA UWONGO NA DUA ZETU ILI UPITE KESI YA UKIMBIZI? LEO SISI NI PUMBAVU NA SHENZI TYPE? 

Kikwete: Nitatumia uzoefu wangu kuiendeleza UDSM.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha  Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, amesema atatumia uwezo na vipaji vyake  kuhakikisha chuo hicho  kinaendelea kuwa bora na kinatoa viongozi wa taifa. 
 
Dk Kikwete aliyasema hayo juzi mara baada ya kumaliza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo chuo hicho.
 
Miradi ambayo ameitembelea Dk. Kikwete ni pamoja na kituo cha mafunzo ya elimu, jengo la sayansi, eneo la maegesho na jengo la mihadhara la Yombo ambalo lina eneo la maktaba mpya.
 
Alisema changamoto ambazo zinakikabili chuo hicho nazo atazifanyia kazi kutokana na kuwa na uzoefu katika serikali kwa miaka mingi. 
 
Aliongeza kuwa atapitia taratibu kwa kuisoma taarifa iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Rwekeza Mukandara, kisha kuitolea majibu kipindi ambacho watakutana tena mwishoni mwa mwezi huu.
 
Dk. Kikwete alipongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuboresha miundombinu ambayo imekuwa kichocheo cha kuongezeka kwa  wanafunzi.
 
Pia alimshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumwamini na kumteua kwa kuwa mkuu wa chuo.
CHANZO: NIPASHE

Kina mama ‘wamzuia’ Magufuli Muhimbili

By Mwandishi Wetu, Mwananchi 
Dar es Salaam. Akina mama waliokuwapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jana walizuia msafara wa Rais John Magufuli wakimtaka kwenda katika wodi ya wazazi ili kujionea jinsi wazazi wanavyokabiliwa na kero mbalimbali ikiwamo ya kulala chini kutokana na kukosa vitanda.
Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa akina mama hao walimsimamisha Dk Magufuli alipokuwa akitoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokwenda kumjulia hali Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir aliyelazwa katika taasisi hiyo.
Baada ya kujionea mwenyewe kero ya msongamano na kuzungumza na baadhi ya wazazi waliojifungua, Rais Magufuli aliwaahidi kuwa atashughulikia kero alizozishuhudia.
“Nimeiona hali halisi mimi mwenyewe, watu wanapata shida, watu wana mateso na ndiyo maana nimeamua kuja kwa makusudi, sikuomba ruhusa ili nijionee hali ilivyo, nimejifunza mengi, ninayabeba na nitajua namna ya kuyatatua,” alisema.

Mbarawa amsimamisha kazi kigogo wa ATCL.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Kasi ya utumbuaji majipu katika wizara mbalimbali nchini imepamba moto baada Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Stephen Kasubi.
 
Kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo kumetokana na kuwepo kwa taarifa za kampuni kupata hasara ya zaidi ya Sh. milioni 700.
 
Mbarawa alisema serikali ilibaini wizi huo kupitia mtandao na wafanyakazi wa ATCL kwa kushirikiana na kampuni ya Salama World Travel iliyoko katika Visiwa vya Comoro.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Profesa Mbarawa alisema: Kutokana na upotevu huo, serikali imechukua hatua thabiti ikiwamo kumsimamisha kazi Kasubi, ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni, ili kubaini mtandao mzima uliohusika.”

ELIMU TANZANIA!

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tegeta A, Kata ya Goba, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakifundishwa na mwalimu wao nchi ya mti kutokana na ufinyu wa madarasa.