dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 28, 2012

Mhe ZITTO AROPOKWA TENA!!!

HUKU NI KUROPOKWA!


Mhe Zitto weka kidole chako chini. 
Zamu yako bado kwanza!
Kuwa kidogo! Labda twenty-twenty!

Ni kweli kuwa hakuna makosa kwa mwanachama wa chama chochote kile kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ya chama hata ya urais, lakini unapotangaza kuwa na ubunge pia hutogombea wakati hujui kama chama chako kitakuchagua wewe au vipi, inatia shaka sana kuwa kuna kitu nyuma ya pazia.  

Bila ya kuwa na fikra mbaya tunategemea kuwa chama cha Chadema tayari kilishakaa na kumpa ishara Nd. Zitto kuwa yeye ndie atakaekuwa chaguo la Chadema pekee hio 2015. Kinyume chake Mhe Zitto ameropokwa! 

Lakini, kwa upande mwengine, kwa Mhe Zitto kuropokwa kama huku sio ugeni kwake. Huko nyuma keshawahi kuropokwa kwa kusema kuwa…“Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa"  na sote tukadhania labda keshajiunga na CCM. 

Mtu anaweza kujitangazia kugombea nafasi ya urais kwa uhakika kabisa kama anataka kugombea as an independent tu, lakini Katiba yetu hairuhusu hivyo. Kama sio hivyo haiwezekani kuwa na uhakika mpaka ukaachia na ubunge. Unavyojiona wewe sivyo wanavyokuona wengine katika chama chako kama wewe sio mgombea pekee. 

ZANZIBAR NI KWETU inasema kwamba Nd Zitto Kabwe amepoteza step na kwa kweli mwenye kupiga vigelegele hivi sasa ni CCM, kwasababu ambazo kila mtu anazijua. Kutokana na huku kuropokwa kwake, possibility ya Zitto kugombea urais kupitia chama chengine pia ni mkubwa sana kwa hivi sasa.

Kugombea urais kupitia Chadema sio sawa na kugombea urais kupitia chama cha Democratic Party au kupitia chama cha Republican Party vya kule Marekani, au hata kupitia CCM. Nia ni moja lakini strategy ni tofauti. CCM mizizi yake imekuenda chini sana na hata kikipigwa na dharuba hakipepesuki ovyoovyo!

Zitto afuate mfano wa Mhe Juma Duni wa kule Unguja na aache mara moja ulafi wa madaraka, kama kweli anataka kula mbivu!

Tuliwahi kusema huko nyuma na tunasema tena na leo pia, kuwa…”Chadema inabidi iyakabili kijitu kizima matatizo ya huyu kijana, bila ya Zitto kudhibiti mdomo wake, chama ambacho kinategemewa na wengi to form the next government in the country will slowly and surely bleed again to an ignominous defeat in 2015!"

Na Geoffrey Kimbitikiri for ZNK

No comments :

Post a Comment