dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 15, 2012

JUSSA APATA KIGUGUMIZI MBELE YA WARIOBA!

Taarifa za hivi punde ni kwamba waziri Mansoor Himid (CCM) ambaye alikuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum, ametimuliwa uwaziri na Rais wa Zanzibar Dr Shein.

Kisa cha kutimuliwa ni kutokana na msimamo wake wa kutaka muuungano wa mkataba jambo ambalo ni kinyume na sera za CCM za serikali mbili.

Chanzo: Jamii Forums

Mhe Jussa, nieleze mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa Mkataba!


Maanake, maanake, maanake, yaani, yaani, yaani......ngoja nikazungumze
na Maalim Seif kwanza!

XXX

Hivyo Jussa kashindwa kumueleza Jaji Warioba kuwa Waznz hawautaki Muungano? Tulieleza zamani kuwa Mkataba is meaningless. Kama tunaona Muungano hauna maana kwetu basi let's say so openly, sio kutaka jambo jengine ambalo tunashindwa hata kulieleza tunapoulizwa. Chakukataa waziwazi ni Muungano. Kitakachofuatia baada ya kufunjika Muungano nobody knows na hakitokuwa chenye Mkataba au Makubaliano yoyote. Wao watakuwa Huru nasi tutakuwa Huru. Why are we mincing words? Why are we making Bw. Matinyi the happiest man on earth today?
Zanzibaris, please, let's make up our minds! It is either YES or NO, but there is NO in-between solution!

/Geo Kimbi
XXX

Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu 

Muungano wa mkataba


Na Mwinyi Sadallah, NIPASHE
15th October 2012
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amembana Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mkongwe (Cuf), Ismail Jussa aeleze kuhusu mfumo wa uendeshaji wa Muungano wa mkataba unavyopaswa kuwa na mgawanyo wake wa madaraka.
Jaji Warioba alichukua hatua hiyo baada ya Jussa kusimama na kutoa maoni ya kutaka mfumo wa Muungano wa mkataba, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya Wawakilishi mjini Zanzibar jana.Alimtaka Jussa atoe mfano angalau mmoja au miwili ya uendeshaji wa serikali ya mkataba ili Tume yake ipate ufahamu katika mapendekezo yake.

Jussa alisema anayo mifano zaidi ya 100 lakini akadai wakati ukifika serikali zinazohusika zitakaa na kuja na fomula ya mgawanyo huo pamoja na uendeshaji wake kimadaraka.

Hata hivyo, Jaji Warioba kwa upande  wake akionekana kutoridhika na maelezo hayo ya Jussa alimtaka kuiambia Tume alivyojiandaa na Muungano wa mkataba kinyume na mfumo dola uliopo.

“Bwana Mwakilishi hebu tupe lau mfano mmoja au muundo wa uendeshaji wa Muungano wa serikali ya mkataba ili uweze kukidhi haja yako na kutuonyesha njia” alisema Jaji Warioba.

 “Hebu tuweke wazi juu ya utashi wa mpango unaofikirika wa kuwa wa serikali ya mkataba, nafikiri unachokusudia ni kutaka kuvunja Muungano uliopo” alisema Warioba.

Hata hivyo, Jussa alibaki katika msimamo wake huku akisisitiza kuhusu kukaa kwa serikali mbili na kutoa mfumo wa uendeshaji wa serikali ya mktaba.

Akifafanua, Jaji Warioba alisema kimsingi kudai Zanzibar iwe na mamlaka kamili, huku Tanganyika nayo ikiwa na mamlaka yake ni sawa na kuvunja muungano kwa kuwa kila upande utalazimika kuwa na kiti Umoja wa Mataifa (UN).

“Tanganyika na Zanzibar zikiwa kila moja ina mamlaka yake hakutakuwa na neno Muungano, ndiyo maana nasema nisaidiwe juu ya kupata mfumo wa kuendesha Muungano unaotakiwa chini ya mkataba” alisema Jaji Warioba.

Akiwekea mkazo katika hoja iliyotolewa na Jaji Warioba, mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo, Paramagamba Kabudi, alisema inasikitisha kuona hadi sasa wanaotaka Muungano wa mkataba wanashindwa kutoa rasimu ya mfano wa serikali ya mkataba ili kuisaidia Tume juu ya kile wanachokitetea.

Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM na CUF waligawanyika pande mbili huku wale wa CCM wakitetea mfumo wa serikali mbili na wa CUF wakitaka Muungano wa mkataba.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha alisema muundo wa Muungano wa serikali mbili ndiyo muafaka kwa kuwa umeonyesha faida katika masuala ya ulinzi na usalama lakini pia ukijenga umoja wa kitaifa.

Akishauri Nahodha alisema hata hivyo ni vyema ikafika mahali kukawa na mabunge mawili , moja dogo litakaloshughulikia mambo ya Muungano na jingine lishughulikie mambo ya Tanganyika.

Aidha alitaka nafasi ya Rais wa Muungano itolewe kwa zamu kila upande uwe na kipindi cha miaka kumi.

“Mgawanyo wa mapato usiangalie idadi ya watu kwa vile hata kama Serikali moja ikiwa na watu wawili bado ina jukumu la kuwapatia maisha bora na huduma wananchi wake” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar Said Ali Mbarouk alisema mfumo wa sasa wa Muungano una matatizo kwakuwa kuna mambo ambayo si ya Muungano lakini yanasimamiwa na Muungano kinyume na makubaliano ya mwaka 1964.

Aliyataja baadhi ya mambo aliyodai yanayoleta mkanganyiko kuwa ni utalii, maliasili, habari na michezo ambayo alisema yanahitaji kuwekewa utaratibu na kuzungumziwa kwake katika medani za kimatifa.

Waziri asie na Wizara Maalum Machano Othman Said alitaka mfumo wa Muungano wa sasa uendelee na kutaka Rais wa Zanzibar kubaki kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza alitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka sawa na Rais wa Muungano pamoja na Zanzibar kupata nafasi ya kujiunga na jumuiya ya OIC na nyingine za kiuchumi duniani.

Tume ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni inayoongozwa na Jaji Warioba ipo visiwani Zanzibar na tayari imekutana na wananchi katika mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba.  

Chanzo: Nipashe!

1 comment :

  1. Sasa wote mbona wanaonekana kukunja mikia ndani? Wale wanaojua kupost kwenye facebook kwamba wanataka kumiliki passport za zanzibar mbona wanaywea teana au kuna mtu anawatisha?

    Jamani kwenye kudai uhuru hakutakiwi kuwa waoga; semeni muungano basi na mtakuwa huru!

    ReplyDelete