dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 23, 2012

MHE PHILIPO AUGUSTINO MULUGO: HUYU ANAFAA HAPA ALIPOWEKWA???


PHILIPO AUGUSTINO MULUGO

Hon. Philipo Augustino Mulugo -- Deputy Minister of Education and Vocational Training, 
Tanzania, speaking on Education for Employment, Developing Skills for Vocation at the 
Innovation Africa Summit - 5th-7th October 2012 at the Westin Hotel, Cape Town, South Africa.
Supported by the Government of South Africa and co-hosted by AfricanBrains and the University 
of the Western Cape.

Deputy Minister for Education and Vocational Training, Philipo Mulugo
Written by   //  23/10/2012 
First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe
EDUCATION:
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys’ High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE CERTIFICATIONS
EMPLOYMENT HISTORY:
Company Name Position From Date To Date
The Parliament of Tanzania Member – Songwe Constituency 2010 2015
Southern Highland Secondary School School Managing Director 2008 2010
Southern Highland Secondary School Administrative & Personnel Officer 2005 2010
Southern Highland Secondary School Teacher 2000 2004
POLITICAL
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member – National Executive Committee 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Secretary General – Mbeya Region (Parents) 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member – Chunya District Political Committee 2007
Chanzo: JF


YA WAZIRI MULUGO SI MAGENI KWETU!

Written by   //  23/10/2012  
Philipo-Mulugo
Siku chache zilizopita, Naibu Waziri wa Elimu Tanzania (sio Tanganyika), Bwana Phillipo Mulugo alivunja mwiko wa ule usemi wa Kiswahili usemao ‘Funika kombe mwanaharamu apite’! Mficha aibu huaibika zaidi, na mdanganya kiaga hudanganya utupu wake. Huu ndio ukweli uliopelekea Waziri wetu huyu kulifunuwa kombe mbele ya mwanaharamu licha ya juhudi kubwa ya kujificha asifanye hivyo. Aibu iliibuka tu.
Sina haja kurudia sana alichokifanya Waziri Mulugo, lakini kwa kukumbushia tu ni kwamba mheshimiwa Waziri alifanya manyanga ya kupigiwa mfano katika historia ya nchi hii mbele ya umati na mitandao ya kimataifa. Kizungu kibovu kabisa, hoja za jongoo bumbwi zisizo macho, papasio wala ndewe za masikio katika mawasilisho yake, sambamba na kufanya makosa makubwa ikiwemo lile baya zaidi la kuitangazia dunia kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili yaani Zimbabwe na Pemba. http://www.youtube.com/watch?v=e3BNegmIUKM
Mdolongo huu wa Pumba hakuna alietegemea kuusikia kinywani mwa hata mwendawazimu muokota makopo aliezaliwa nchi hii miaka 48 iliyopita, sembuse Waziri mwenye dhamana nzito ya Elimu nchini. Mimi kama mwandishi hapa Mzalendoni sitaki nimhukumu Waziri Mulugo nitaitwa CUF au Uamsho, lakini kama kuna mtu aliwahi kuona katika Blogu kama vile michuzi, ataona jinsi gani watu wa huko kwao Bara walikvyokerwa na hutuba na upeo mdogo alionao Waziri Mulugo. Kule Youtube ndio kabisa, na laiti ingekuwa Video ile ingemhusu kiongozi au mtu maarufu wa huko majuu basi ingekuwa balaa. Lakini hata hivyo yaliyotokea na ujumbe utakuwa umemfika Rais na Waziri wetu wa Elimu Bwana Mulugo.
Binafsi sishangai kwa watendaji wetu wakuu kuwa wabovu si kwa kuongea kimombo tu, bali hata ule uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja hawana. Viongoiz kadhaa wa huko Bara yamewakuta haya wakiwa ughaibuni lakini ndio kombe hufunikwa mwanahizaya akapita. Hapa Zanzibar tuliona enzi za Sheikh Karume(Amani) pale Naibu Waziri wa Afya alipoakikataa mialiko mingi ya nje na ikawa anamuchiwa Bi. Asha Abdalla Juma (Tom Boy) aende mikutano hiyo ya kimataifa. Kisa? Bibie alikuwa hajui jambo ni ‘pyoro’ wa ukweli.
Serikali zetu zote mbili hapa Tanzania hazitafuti watu kwa mujibu wa uwezo wao. Bali hutafuta watu ili nao waje wajipatie rizki zao ili wasikose kijipande kidogo cha historia cha kusema ‘Kaka alipokuwa Rais, nilikuwa Waziri bwana’. Haya ndio maneno yanayotafutwa. Serikali zimekuwa za kijomba jomba mno na za kisiasa zaidi kiasi ambacho hata huko nje tunachekwa na kusimangwa bila kujijuwa. Suali la aibu alilofanya Mulugo limetutia doa na kutuvua nguo kusema kweli mbele ya medani za kimataifa na hasa ndugu zetu wa Kenya, ambao kimsingi hutuona matobwe sana katika kuendesha nchi. Tabia hii inaiondolea heshima Serikali kwani huonekana ni kichaka kidugu cha wahuni badala ya watu wenye upeo mkubwa wa kuendesha nchi na kuleta maendeleo.
Lakini yote haya ni matunda ya Muungano na uvyama kuwekwa mbele zaidi kuliko maslahi ya taifa. Tanzania hii ina watu wenye uwezo sana kiuongozi wa nafasi aliyonayo kama huyo Mulugo au aliekuwa naibu waziri wetu wa Afya 2000-2005 ambae jina lake ni la tunda liitwalo Embe huku Unguja. Nakumbuka Rais Kikwete ameshabadilisha baraza mara kadhaa, lakini kila uchao ndio hivyo hivyo. Akiacha kuchaguwa bovu, huchaguwa bokerewa. Na hii ni kwa sababu hana hao wa kuwachaguwa kwa vigenzo walivyoweka wao. Maana kuna lazima atoke chamani tena awe ‘hewalla Bwana’ sasa alie msomi wa kweli hayo hayakubali.
Upigwavyo ndivyo uchezwavyo. Na sisi hatuna budi tuucheze hivi hivi wanavyoupiga, siku ikipasuka kila mtu atatafuta njia yake aende lakini suali linabakia kuwa Mustakabli wa Taifa hili hautaimarika wala kuboreka iwapo tutaendelea kuchaguwana kwa misingi ya udugu, kisiasa, na kiuvyama. Tutabakia kuwa vizuu na misukule ya kuuwana wenyewe huku wajanja wakihujumu uchumi wan chi yetu tunaowaachia kwa hiari zetu. Na kwa mtindo huu hatufiki popote! Hongera Waziri MULUGO! Huna lawama, na atakekulaumu mnyooshe kidole bosi wako aliekuteuwa akiamini kuwa lawama zote za uteuzi wake ni zake yeye mwenyewe.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment