dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 13, 2013

MOBHARE MATINYI: Mapendekezo ya Katiba kutoka Chadema

Above: Mobhare Matinyi - a revolutionary dictator!

Hapa chini tunatoa comments za Bwana Mobhare Matinyi ambae ni Consultant huko Washington DC juu ya mapendekezo yaliyotolewa na chama cha Chadema. Bwana Matinyi anaandika sana katika gazeti la The Citizen. Yeye ana-column yake inayotoka kila Ijumaa chini ya title ya 'The Eagle's Eye', ambayo kwa Ijumaa mbili mfululizo sasa haijatoka. Hii inaashiria kuwa labda Mhariri wa The Citizen hakubaliani na fikra za Bw. Matinyi anazozitoa kwenye hii column kila Ijumaa - fikra ambazo mara nyingi zinakuwa za upande wa kushoto sana.
Bw. Matinyi ni mzalendo sana na anaipenda Tanzania kuliko kitu chochote kile (kama sisi sote) na yupo tayari hata kwa nguvu kuhakikisha kuwa Muungano wa Tanzania unabakia kama ulivyo - yaani wa serikali mbili au unageuka kuwa wa serikali moja. Fikra zake yeye juu ya Muungano ni kama za yule muandishi mwengine wa Bara anaejulikana kwa jina la Absalom Kibanda ambae bila ya haya amewahi kutamka huko nyuma kuwa eti..." Ni uendawazimu kufikiria kuuvunja Muungano. Ni usaliti wa utaifa wetu. Ni upotofu usiovumilika na kimsingi ni uasi unaopaswa kujibiwa na kuzuiwa kwa nguvu zote kwa namna ile ile aliyofanya Abraham Lincoln". Haya ndio wanayoyaandika waandishi wetu na ma-Consultants wetu.
Eti ni uendawazimu kuuvunja Muungano ambao unawarejesha nyuma wengine - Muungano ambao unapunguza the quality of lives of Zanzibaris! Gazeti lake yeye mwenyewe Bw. Matinyi - The Citizen, la tarehe 13 January, 2013 linaandika..."As Zanzibaris celebrate the 49th anniversary of the Revolution, analysts are of the view that the quality of lives of the Islanders have been hampered partly by the Union with Tanganyika". Ikiwa ni hivyo, Bwana Matinyi na Bwana Kibanda, vipi itakuwa uendawazimu na usaliti wa Taifa kuuvunja Muungano huo, vipi tutaweza kujibu kwa nguvu zote nia za wale ambao wanataka kunyanyua the quality of their lives?
Hivyo kutaka kunyanyua the quality of lives of the Islanders ni uendawazimu, ni usaliti na ni lazima ukabiliwe kwa nguvu zote?
Sisi tunasema kuwa, uendawazimu ni ule wa kusema kuwa Rais wa Muungano asitoke Zanzibar kwasababu inayo watu kidogo.Tukisema hivyo leo basi kesho tutasema Rais wa Muungano atoke katika kabila la Wasukuma kwasababu ndio wengi na keshokutwa tutasema kuwa Rais wa Muungano atoke katika kabila la Wachaga kwasababu ndio waliosoma sana. Hapa, hapana wingi wa watu, hapana kabila kubwa na wala hapana wepi wamesoma sana. Hapa ni kupokezana baina ya nchi mbili zilizoungana hata kama moja ni ndogo kama kifuu au inayo watu wawili tu - ikifika zamu mmoja ya watu wawili hao apewe urais madamu anauweza!
Tunajua Bw. Matinyi atauliza kama alivyouliza huko nyuma kuwa...'Je, ni busara kweli kuwa na urais au nafasi nyingine nyeti, kwa kupokezana kwa nchi ambayo rais ni kila kitu kutokana na umaskini na ujinga wetu?' Jibu ni kuwa sio busara, lakini Wazanzibari wa leo sio wale wa 1964. Leo tumesoma na tunaiweza nafasi nyeti yoyote ile katika Muungano. Na kama kazi yenyewe ni kama hio ya JK ya kuwa hewani kila siku, basi Bwana Matinyi usiwe na wasiwasi hata kidogo, kwani tutaiweza tu. Hatutokubali kuwa katika Muungano ambao kazi yetu sisi kubwa itakuwa as 'the hewers of wood and drawers of water'! 
Wote hawa - Bw. Matinyi na Bw. Kibanda ni watu wakorofi wasioitakia mema Zanzibar na bila ya shaka wameshitushwa kuona kuwa Chadema pia imetambua kuwa Muungano tulionao hivi sasa umepitwa na wakati na ipo haja ya kuubadilisha.
Sisi kama Zanzibar Ni Kwetu tunaipa heko Chadema na japokuwa hawajafikia tunakotaka wafike, but they are on the right track!
Tunahakika kuwa kama Chadema wakiingia Ikulu basi we will be able to iron out the few bugs that are still conspicuous. Tunahakika sio Chadema wala sio sisi wenye nia ya kuuvunja Muungano. Nia yetu sote ni kuufanya Muungano/Uhusiano wetu uwe wenye kukubalika kwa pande zote mbili na uwe sio ule wenye kupunguza quality of lives kwa upande mmoja. 
Bwana Matinyi na jamaa zake wa mlengo wa kushoto wanataka Muungano wetu uegemee upande mmoja tu - jambo ambalo kwa dunia ya leo halikubaliki, kwasababu huu ni Muungano wa nchi mbili huru na sio wa nchi moja na jimbo fulani!

00000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000
Mobhare Matinyi
Washington, DC
January 13, 2013.

Tundu Lissu,

Ninashukuru kwa salamu zako za mwaka mpya pamoja na kutuwekea maoni mliowasilisha kwenye Tume majuzi. Mimi niliyasoma pale pale ulipoweka tu na kisha nikapanga kwamba niyasome tena na kujaribu kupitia kipengele kimoja kimoja kwa kuwa nami ninaandaa maoni yangu binafsi ya kutuma kwenye Tume. Lakini kabla muda haujasogea sana, naomba niseme haya mawili matatu ili nisije nikashindwa kutimiza lengo langu la kutoa changamoto:

Kwa kuangalia ile picha nzima yakiujumla ya falsafa ya maoni ya uongozi wa Chadema, kuna jambo moja ninalolipongeza na moja nisilokubaliana nalo.

PONGEZI
Kwamba maoni ya Chadema yameliona tatizo moja kubwa barani Afrika - nalo ni lile la mfumo wa mshindi wa uchaguzi kuchukua kila kitu. Hapa Afrika uchaguzi una maana zaidi ya moja kulinganisha na wababe waliotulazimisha kuendesha nchi zetu kwa kufuata mifumo yao. Uchaguzi Afrika si siasa tu, bali pia ni uchumi, utamaduni, dini, jamii, n.k. Anayeshinda uchaguzi anaonekana kwamba amepata ulaji, yeye na walio nyuma yake na ndio maana ukabila huzisumbua nchi zetu, na hali kadhalika udini, na migawanyiko mingine. Ushindi wa kura ni ushindi wa kula. Bahati mbaya sana.

Suala hili mmeling'amua vema na kulifanyia kazi ambapo iwapo maoni haya yatakubalika, basi wanaoshindwa kwenye chaguzi mbalimbali watakuwa na fursa ya kupata ama kuingia kwenye uwakilishi mwingine wa chini kidogo kutokana na asilimia ya kura walizopata. Naomba nisitoe mifano ili watu waende kusoma wenyewe maoni yenu ambayo yamekuwa mafupi kuliko nilivyotarajia kwa kweli - tuacheni uvivu wa kusoma.

Mfumo huu mlioushauri unaleta tumaini kwa wanaoshindwa na kuzuia hamu ama kubana sababu za kuleta fujo kwa kuwa tu mgombea na watu wake wanaona wamepigwa bao kwa miaka mingine mitano tena. Angalia Ghana, jamaa amepitwa kwa asilimia pungufu ya moja, ndiyo haifiki hata moja, lakini yeye na watu wake (sijui kabila lake, ama dudu gani sijui), hawatapata kitu kwa miaka mingine minne huku mwaka 2008 alipitwa kwa asilimia mbili ama tatu na akakosa "ulaji" kwa miaka minne. Hii inauma na inaweza kuilipua nchi na ndiyo maana wapinzani wamemsusia rais mpya. Hivyo, falsafa hii ya kuzuia mshindi wa kura ili asiichukue keki yote inahitaji pongezi. Itaihakikishia nchi yetu amani chini ya mfumo huu wa vyama vingi ambao akili zetu Waafrika haziwezi kuuelewa hata kwa dawa gani. Hatuko kihivyo. Huenda panahitajika marekebisho, lakini kwa kuanzia hapa ni pazuri. Tunahitaji taifa lenye amani na tumaini.

KUTOKUBALIANA
Kwenye mfumo wa Muungano uongozi wa Chadema umependekeza kwamba kuwe na serikali tatu: Bara (wametumia neno Tanganyika), Zanzibar na ya Muungano (Shirikisho). Wamependekeza kwamba mambo ya Muungano yawe saba huku polisi na magereza vikiwa nje ya Muungano. Wamesema pia kwamba suala la uhusiano wa kimataifa lisiwe la muungano bali diplomasia tu ndiyo ibakie kwenye muungano. Wanataka serikali ndogo ya Shirikisho na serikali mbili za Bara na Zanzibar zenye nguvu kubwa mno kuliko ile ya Shirikisho ambayo pia Rais wake atateuliwa na mkusanyiko wa vikao na watu kibao kama ifuatavyo: "Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote."

Hapo kwenye wenyeviti, mameya na magavana - naomba mkasome wenyewe kwenye mapendekezo ili muwajue.

Kwa nini sikubaliani na pendekezo hili? Ingawa mfumo wa serikali tatu - shirikisho - unawezekana, lakini huu unaopendekezwa hapa hauna mantiki kiutendaji kwa kuwa:

1. Unaifanya serikali ya shirikisho kuwa kaserikali ka ujanja ujanja na kadhaifu chini ya serikali za sehemu mbili za Muungano. Hakuna hata nchi moja duniani iliyowahi kuwa na mfumo huu na kufanikiwa kusimama. Pale Wasovieti walipojaribu tu, ndiyo ulikuwa mwisho wa Muungano wa Jamhuri za Kijamaa za Kisovieti (USSR). Hii ilikuwa baada ya Mikhail Gorbachev kushika madaraka na kujipendekeza kwa sera za magharibi. Mataifa yote yenye mashirikisho, ngoja niyataje, Sudan, Nigeria, Afrika Kusini, India, Pakistan, Ujerumani, Kanada, Meksiko, Brazil, na Marekani, serikali zake za mashirikisho ndizo zenye nguvu. Hatuwezi kufanikiwa kwa kuwa na serikali dhaifu ya shirikisho. Lengo letu ni kuulinda muungano na si kuweka mazingira mazuri na laini na mepesi ya kuuvunja kama mapendekezo haya yalivyofanya. Napinga.

2. Serikali ya Muungano ya kishirikisho itakuwa na mambo haya kwa mujibu wa mapendekezo hayo:(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa; (b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza; (c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic); (d) Uraia na uhamiaji; (e) Sera za fedha na sarafu; (f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha; (g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.

* Tatizo liko wapi? Hatuwezi kushirikiana katika diplomasia halafu kila nchi ikajitegemea kwenye ushirikiano wa kimataifa. Nadhani hapa pia kulikuwa na tatizo la kutokujua maana ya diplomasia. Diplomasia ni nini? Diplomasia ni sanaa ama ujuzi ama ufundi ama mbinu - yaani kifaa tu cha kushughulikia masuala ya uhusiano/ushirikiano wa kimataifa. Labda nitoe mfano kidogo. Sufuria siyo chakula bali ni chombo cha kupikia chakula. Huwezi kusema kwamba tuishi pamoja na tushirikiane kwenye sufuria lakini kwenye chakula kila mtu na vyake. Haina maana. Mfano mwingine. Uwanja wa Taifa si mchezo wa soka bali ni kitu kinachotumika kuchezea mchezo wa soka, kwamba bila uwanja ule hatuwezi kucheza soka. Hatuwezi kusema kwamba tushirikiane uwanjani, lakini kwenye soka kila mtu na lwake. Haina maana. Sasa ni kwenye nini ndipo tutakuwa na muungano wa diplomasia ambapo si mahala pa ushirikiano wa kimataifa? Nadhani hapa Chadema hawakujua wanazungumzia kitu gani na nafikiri kama Prof Baregu angekuwepo kwenye timu ya Chadema (sasa yumo kwenye Tume), angetoa somo kwenye jambo hili. Kwa kifupi, hakuna kitu kama hiki - hii ni sawa na Maalim Seif kudai kwamba kuna mnyama anayeitwa "muungano wa mkataba." Hakuna vioja kama hivi duniani. Labda ilikuwa ni njia ya kuukwepa mjadala wa OIC. Haiwezekani.

* Je, kila nchi ikifanya mambo yake ya ushirikiano wa kimataifa, hali itakuwaje? Ni kwamba EAC au SADC au AU au UN wakiitisha kikao zinakwenda Tanzania mbili. Zanzibar inaweza ikajiunga na Arab League (kama Somalia) huku ikisema kwamba "Tanganyika" wao hawamo kwa kuwa si Waarabu na sisi tukajiunga na OIC na kusema kwamba "Zanzibar" wao hawamo kwa kuwa wanafaidi sana kule Arab League. Dunia nzima itatuona wehu. Kwamba itabidi, ndani ya nchi moja, kuwe na balozi za nje Dar es Salaam na pia ziwepo za kule Zanzibar na kwamba itafika mahali sisi tutasema kwamba hatutaki uhusiano mathalani na Iran lakini tunataka na Israel na Zanzibar wao wakasema kwamba wanataka uhusiano na Iran lakini hawataki na Israel, na kisha tukasimama mbele ya dunia na kusema hili ni Shirikisho la Tanzania. Huu ni mzaha mkubwa na watu watatuona majuha. Hakuna kitu kama hiki duniani na hakiwezekani. Napinga.

* Kwenye masuala saba ya Muungano kuna tatizo moja ambalo nchi zote zenye mfumo wa shirikisho zililiona na kulikwepa, nalo ni ukweli kwamba HAKUNA SERIKALI NUSU MKATE HAPA DUNIANI. Serikali ni chombo kamili kinachosimamia mambo yote; hivyo huwezi kuwa na serikali inayosimamia mambo saba na kuyaacha mengine yote kwenye serikali mbili ambazo hazina "sovereignty". Hebu fikiria suala hili, kwamba UNESCO inataka kutiliana saini na Tanzania kwenye suala la utamaduni na sayansi. Kwa kuwa haya si masuala ya Muungano, itabidi serikali ya Shirikisho ikae kando kwa kuwa haina hata wizara yake. Nani atatia saini kati ya waziri wa Zanzibar na Tanganyika? Haya ikija FAO na WFP za masuala ya kilimo na chakula je? Ikija UN Habitat kwenye masuala ya makazi? Ni nani atakuwa anakwenda nje kujadiliana kuhusu masuala yasiyokuwa na Muungano na nani atakuwa anatia saini na hao wanaozungumza na sisi, watasema wameongea na nani? Tanzania au vi-inchi vya Tanzania? Huwezi kuwa na serikali nusu-mkate. Napinga.

Masuala mengine ni mazuri ila yanahitaji kupitiwa tena, mfano muundo wa mahakama nao una tatizo kwa kuwa unaiminya mno mahakama ya juu kabisa ya shirikisho kwa kufuata falsafa ile ile ya kuidharau Tanzania na kuzikuza Tanganyika na Zanzibar. Hili silikubali pia.

Suala la mfumo wa serikali za majimbo kumi unahitaji kuangaliwa upya, hasa kwenye mgawanyo na ulazima wa nambari "KUMI" ambayo siijui ulazima wake. Kwa nini isiwe TISA au KUMI NA MBILI au mikoa ya zamani (achana na hii mipya ambayo siielewi ulazima wake)? Palihitajika maelezo ya kina kuhusu dhana nzima ya uundwaji upya wa serikali za mikoani/majimboni na wilayani zinazowajibika kwa wananchi moja kwa moja. Hapa panahitaji kazi zaidi lakini ni mwanzo ni mzuri.

Niishie hapa. Nalipongeza sana wazo la kuzuia watu kugombea ulaji kwa mlio wa kura; lakini nalipinga suala la kuifanya serikali ya muungano kuwa dhaifu, kuwa nusu-mkate na kuandaa mazingira poa ya muungano kuvunjika kiulaini, kwamba upande mmoja wakipiga kura tu, ngoma kwisha. Hapana!

Tunashukuru kwa uzalendo wenu.

Matinyi.


Chanzo: Wanabidii Forum 

No comments :

Post a Comment