dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 11, 2014

FAMILIA YA JK YAHUSISHWA NA UFISADI

Written by Makengeza  //  11/11/2014; Mzalendo.net

Kichwa lazima kiume, kwani haya sio madogo!

Ufisadi wa dola 250m (zaidi ya 400bn) umetikisa nchi kwa kuikosesha takribani miradi ya sh 3trilion imefahamika. Kampuni ya PAP ilipewa dola 122m (200bn), na kusaini makubaliano kikao cha kunduchi beach hotel oct8.2013 kuwa kiasi kilichobaki (128m au zaidi ya 200bn), PAP watalipwa
kila mwezi 8bn mpaka deni kwisha.
Kampuni hii ya PAP iliyopewa tuzo hiyo ya 400bn kwa kuwekeza 6mTsh tu ni ya nani? Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, 50% inamilikiwa na Singh Sethi(singasinga) na mwanae na asilimia 50% zinamilikiwa na kampuni ya
Simba Trust ya Australia.
Simba trust ni ya nani.? Uchunguzi umeonesha kuwa Simba trust ya Australia inamilikiwa na watu wawili ambao ni Salima Kikwete na Miraji Kikwete.
                 Kufikiria kufungua kampuni Australia! Hio ni kweli mama - bongo imetumika!
Uwepo wa majina haya mawili kama wamiliki wa PAP inatafsiriwa kuwa ndio sababu kuu ya JK kuvuta miguu huku nchi ikiumia.
Kwa mkataba huu wa IPTL wa 100MW wa miaka 20 (1995_2015), umeongezwa miaka mingine 20 (2013_2033)kwa kuzalisha 500MW.
Kwa mujibu wa mkataba huu, kampuni ya PAP italipwa 400m kila siku kama capacity charges . Maana yake singasinga mwenye 50% atapata 200m kila siku.
Na watoto wawili wa JK watapata kila mmoja 100m kila siku hadi 2033.
Uwepo wa familia ya JK kwenye ufisadi huu inadaiwa ndio Kinga ya wahusika; Muhongo, werema, maswi, mramba, likwilile na hata waziri mkuu Mizengo Pinda.
Ushahidi unakwenda kuonesha kuwa hata uamuzi wa Gavana kuruhusu fedha hiyo itoke kimakosa ni baada ya kupata MEMO kutoka Katibu wa rais Bw Mbena
ikisema Rais kaelekeza.
Na ni sababu hiyo pia baada ya Dr Hosea kuwasilisha report kwa rais, JK alisoma na kumjibu achana nayo na ndio maana mpaka sasa report hiyo haijapelekwa kwa DPP ili wahusika wafikishwe mahakamani. 
Ukweli utasimama!


No comments :

Post a Comment