dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 10, 2014

QABOOS AJENGA MSIKITI MKUBWA ZANZIBAR - 1!

  • Msikiti unajengwa Mazizini opposite na kituo cha polisi
  • Ujenzi wa ‘Masjid Qaboos’ kukamilika 2016.
  • Na Hafsa Golo


    Sultan Qaboos wa Oman.
Msikiti mkubwa unaojengwa na Mfalme Qaboos wa Oman ambao una uwezo wa kusaliwa na waumini zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja, umefikia hatua nzuri ya ujenzi wake na na unatarajiwa kukamilika mwaka 2016.Hayo yamebainika wakati Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Juma Shamuhuna, alipotembelea msikiti huo kuangalia ujenzi unavyoendelea.

Meneja wa mradi wa ujenzi wa msikiti huo, Mhandisi, Ahmed Khalfan Al-shukaili, alisema ujenzi ulitarajiwa kukamilika mwaka ujao lakini haitowezekana kwa sababu ya kuchelewa baadhi ya vifaa.

Aidha alisema msikiti huo unajengwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha unadumu kwa zaidi ya karne moja bila kujitokeza athari.

“Msikiti tunaojenga utapendeza kama Mfame alivyoagiza na Mwenyezi Mungu akijaalia utadumu milele bila kujotokeza hitilafu,” alisema.

Naye Waziri Shamuhuna, alisema msikiti huo pia utakuwa na chuo cha kiislamu kitakaochukua zaidi ya wanafunzi 100 kwa wakati mmoja.

Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Mazizini, Dk. Muhyddin Ahmad (Maalim Siasa), alisema iwapo chuo hicho kitaanzishwa wanafunzi watafundishwa na walimu wazalendo.

Alisema wapo walimu wanne wenye shahada ya uzamivu (Phd) na 21 shahada ya uzamili na kwamba walimu 18 wako masomoni nje ya nchi wakisomesha shahada ya uzamili na uzamivu.


Huo msikiti utakaojengwa Zanzibar hautokuwa mkubwa kama huu wa huko Oman unaotarajiwa kumalizika karibuni, lakini sio utakuwa mdogo pia kwa Zanzibar. 
Tumshukuru Qaboos kwa msaada huu na tumtakieni kila la kheri katika matibabu yake huko Ujerumani hivi sasa!

No comments :

Post a Comment