dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 29, 2014

SERIKALI YA MUUNGANO IMESHINDWA KULINDA HAKI ZA WANANCHI!

Outreach Clinic
A Clinic in Arusha!
Prof Tibaijuka na Ndugu Chenge - nyinyi ni watu wenye huruma, tafadhalini turejesheeni japokuwa khamsini elfu kila mmoja kutoka hizo bilioni 1.6 mlizogawiwa kwa kila mmoja wenu ili tupate kuwajengea a proper clinic hawa ndugu zetu wa Arusha!

(Zanzibar) - Kusimama kwa Waziri wa Nishati na Madini bungeni Prof Muhongo (ambae wengi wanamjua hapa Visiwani kwa jina lake la utani kama Prof Muongo) na kuutetea wizi uliotendwa na baadhi ya mawaziri na wenye vyeo vya juu serikalini kwa kupokea pesa haramu, kumeifanya serikali ya Muungano ionekane hapa Zanzibar kama ni serikali ambayo haiwezi kulinda haki za wananchi au kujali hali za wananchi wake nchini.

Wengi wetu hatufahamu vipi Waziri mwenye akili timamu anaweza kusimama mbele ya wabunge na kusema kuwa, "hizo pesa lakini zilikuwa sio za umma". Kwa kweli Prof Muongo kajifanya kuwa mtu sio wa maarifa. He is the least person to be expected to say such a stupid statement. Yeye ni mtu aliesoma na sio ngumbaru kama sisi wengine, lakini penye pesa inaonesha elimu yote hupotea na tamaa ndio huongoza!

Zanzibar Ni Kwetu kama ilivyoahidi iliendelea kuwahoji Wazanzibari kutoka sehemu mbali mbali ya mji wa Zanzibar, ili kupata maoni yao kutokana na wizi huu wa mchana uliofanyika kutoka kwenye akaunti ya ESCROWGATE.

“Hii ni serikali yenye wasomi wengi na wengi kati yao ni ma-Profesa wenye PhDs, lakini shahada zao na uprofesa wao wote ni kuelekea kwenye kula tu na kutuibia sisi wananchi. Hivyo hio faida ya gesi itaonekana kweli jamani ikiwa wizi serikalini unaongozwa na mawaziri wenyewe ambao tunategemea watakuwa waaminifu?”, alitaka kujua kijana mmoja wa hapa Darajani, Zanzibar, pale alipoulizwa nini yalikuwa maoni yake kutokana na hili sakata la ESCROWGATE?

“Mimi ni mwanachama hai wa CCM na unaniona nimevaa shati la kijani. Hii ndio uniform yangu, kwani kila siku kama sio shati la kijani basi suruali au kofia yangu itakuwa ya kijani. Hii inaonesha uaminifu wangu kwa chama changu cha CCM, lakini kama waliogawiwa pesa watabakia serikalini na hata kama watabadilishiwa kazi na kupewa za ufagizi maofisini basi kura yangu ya 2015 itakuenda chama chengine na sio CCM tena”. Hayo aliyaeleza Mzanzibari mwengine ambae mpaka sasa alikuwa mpenzi wa CCM na anabiashara zake pale Darajani.

“Kama hawa waliogawana pesa wataendelea kuwemo serikalini basi hata na mimi sitoipa kura yangu CCM mwakani”, haya aliyasema Mzanzibari mwengine ambae alikuwa akifanya shopping pale Darajani akijitayarisha kusafiri kuelekea Dubai kwa shughuli zake za kibiashara.

"Kinachoniuma mimi zaidi ni kumuona Prof wetu wa kike ambae wengi katusomesha na tukimuamini kuwa ni mpiganaji wa walalahoi akiwemo katika kundi la mafisadi wa nchi hii. Kama wanavyosema wahenga kuwa, penye pesa hutomjua baba, mama, fisadi au mwema - wote wanakuwa mafisadi - hii sasa imedhihirika kuwa ni kweli kabisa", alimalizia huyu kijana anaetaka kusafiri karibuni.

Kutoka Darajani moja kwa moja muandishi wa Zanzibar Ni Kwetu alielekea soko la Mwanakwerekwe la hapa mjini Zanzibar na huko alikutana na mwanamama mmoja ambae alikuwa chakari akipiga mayoeyoe, kama vile alifiwa na mumewe na huku akisema kwa sauti ya unyonge,
” Tumekwisha, tumekwisha, tumekwisha”. 

Alipoulizwa, tumekwisha vipi mama? Yeye alijibu, “Sasa tumefika pabaya. Baba hamjui mtoto, mama hamjui mwanawe na mawaziri hawajui kitu chengine isipokuwa ni KULA, KULA, KULA tu. Dawa ni kuwa kila aliegawiwa pesa hata kama ni centi mmoja basi aturejeshee na serikali ya Muungano aione paa na jela akatumike maisha”, alieleza mama huyu. 

Alipoulizwa na Zanzibar Ni Kwetu kwanini amekuwa na msimamo mkali kama huo, yeye alijibu, “Bila ya kuwapa adabu ambayo itakuwa mfano kwa mawaziri, majaji, ma-askofu na wachungaji wengine, basi siku zote wananchi wa nchi hii watakuwa wakiibiwa”, alimalizia mama huyo na huku azana ya al asr ikisikika. Wakati muandishi wa Zanzibar Ni Kwetu akikimbilia msikitini kusali wananchi tele waliizunguka gari yake wakimngojea ili wampe maelezo zaidi kuhusu misimamo yao ambayo tutaitoa kwenye makala ifuatayo.

Pia soma: http://www.zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2014/11/wazanzibari-nao-wajajuu-kuhusu-kuliwa.html

No comments :

Post a Comment