dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 27, 2014

WAZANZIBARI NAO WAJA JUU KUHUSU KULIWA KWA PESA ZA AKAUNTI YA ESCROW!

  • ·         Wataka wote waliokula pesa wapigwe risasi hadharani.
  • ·         Waeleza kuwa hii ni sababu moja zaidi ya kutaka serikali 3.
  • ·         Wasema kesi hii itakuwa kipimo cha kumpima JK na CCM.
Dada Tibaijuka na Mzee Vijisenti, tunaomba laki moja moja tu mturejeshee katika hizo bilioni 1.6 kila mmoja alizotiliwa kwenye akaunti yake, tupate kuwajengea banda la kuku hawa watoto ili ikinyesha mvua wasipate kuvunja darasa na kurejea nyumbani!

(ZANZIBAR) - Kutokana na kashfa  ambayo imetoa siri na majina ya wale waliokula fedha nyingi sana kutoka akaunti ya ESCROWGATE kama inavyojulikana hapa mjini Unguja, blog la Zanzibar Ni Kwetu lilipita mitaani na kutaka kujua Wazanzibari wanasema nini juu ya huu wizi.

Kama Watanzania wengine huko Bara, Wazanzibari nao wamekuja juu na wanafoka, kwani wameshitushwa na kukerwa sana juu ya huu wizi, hasa kwavile mahospitalini hivi sasa hakuna dawa na wala hakuna vitanda na wagonjwa wanajazana wakilala chini kwenye sakafu kama samaki wakubanikwa na shule nyingi hazina madawati na watoto wanasoma chini ya mibuyu kama watoto wa wakimbizi.

“Madamu majina yanajulikana na uhakika upo wa kuwa walikula pesa za hii akaunti la kufanya ni moja tu”, alisema mzee mmoja wa Muembe Njugu kutoka hapa Zanzibar. Alipoulizwa na Zanzibar Ni Kwetu hilo moja la kufanya ni nini? Kwa ukali mzee alijibu, “ kubadilisha baraza la mawaziri peke yake haitoshi, ila wote waliokula pesa za akaunti hii wachapwe risasi hadharani, ili tuumalize mzizi wa fitna. Kama ingelikuwa China hili lingelikuwa suala dogo tu na hukumu yake ingelikuwa mfano mzuri kwa mawaziri na wakubwa wengine, lakini hapa kwetu tutalindana tu”.  Aliendelea huyu mzee na huku akisikitika kwa kutingisha kichwa chake kama ng’ombe dume aliekosa malisho.
“Kama huyu Chenge jamani ni mara ya ngapi hii anatuibia? Siku zile alivyokamatwa kwenye pesa za Radar akasema eti zilikuwa vijisenti tu alivyovichukua, je, leo atasema nini? Maanake bilioni 1.6 sio pesa kidogo. Wataendelea kumlinda na safari hii pia?”, akamalizia huyu mzee machachari.

Kijana mmoja ambae pia hakutaka jina lake litajwe ambae anaishi Michenzani yeye alisema, “ Wale Wazanzibari wapofu sasa watajua kwanini tunataka serikali 3. Nchi hii haitokuja juu asilan. Ona sasa, EU imesimamisha misaada yote mpaka ile ambayo ingelikuja Zanzibar, kutokana na huu wizi wa hii akaunti ya  ESCROWGATE. Haya yasingelitufika kama kila mtu angelikuwa na serikali yake kamili”, alimalizia kijana.

“Vipi waziri atakubali atiliwe kwenye akaunti yake
 bilioni 1.6 wakati wananchi wanakufa njaa?” Aliyaingilia kati mazungumzo yetu kijana mmoja ambae alikuwa pembeni akitusikiliza. “Sasa kweli tutajua kama hii CCM ni CCM au ni Chukua Chako Mapema, kwani hukumu ya wezi hawa itakuwa ni kipimo tosha juu ya CCM na juu ya Rais wetu. Je, Chenge ataachiwa na hivi vijisenti vya bilioni 1.6  kama alivyo achiwa kwenye wizi wa Radar?”, aliuliza kijana na kumaliza maneno yake wakati huku jua nalo lilikuwa likipotea.

Zanzibar Ni Kwetu itaendelea kupitapita mitaani hapa Zanzibar kujua zaidi nini Wazanzibari wanasema kuhusu huu wizi wa mchana na hukumu gani wanataka walioiba wapewe.

Pia soma hapa: http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2014/11/serikali-ya-muungano-imeshindwa-kulinda.html

No comments :

Post a Comment