dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 28, 2015

WANA-CCM KUTOKA PEMBA KUENDA MONDULI KUMRAMBA NYAYO LOWASSA ILI AGOMBEE URAIS 2015!

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Wimbi la kumshawishi Lowassa kugombea lapamba moto.

28th February 2015
Wimbi la watu kumuunga mkono na kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kugombea nafasi ya urais wakati utakapofika, limezidi kupamba moto na safari hii, ujumbe mzito kutoka Pemba unajiandaa kufanya hivyo.

Taarifa za maandalizi kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Pemba kwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea urais, zimekuja siku chache baada ya baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kanda ya Ziwa, kufanya hivyo wiki iliyopita.

Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, walimtuma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Monduli jana,  Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa, (NEC) kutoka Wilaya ya Chake Chake Pemba, Daud Ismali, alisema amekwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea nafasi ya urais muda utakapofika.

Ismail ambaye ni mdogo wa Makamu wa Rais, marehemu, Dk. Omar Ally Juma, alisema kwenda kwake Monduli kufanya maandalizi ya ujumbe mzito utakao toka Pemba kwenda kumshawishi agombee urais.

"Watakuja kumwomba mheshimiwa Lowassa kugombea urais, uamuzi wa kugombea au kutogombea ni wake".
Akieleza kwanini waje kumshawishi Lowassa badala ya mtu mwingine, alisema ni kutokana na utendaji na uadilifu wake.

Pia alisema, “jina la mheshimiwa ni kubwa na siyo Pemba tu hata ukienda Marekani ukiuliza ni jina gani linazungumzwa kuhusu urais utaambiwa ni Lowassa.”

“Ukienda mtaani kukusanya data za aina yo yote ile, jina linalotajwa kuwa linafaa kuwania nafasi hiyo ni la Lowassa,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment