dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 30, 2015

Wanaharakati wapinga muswada wa mtandao

Image result for logo of Shirika la Sikika
WADAU wa matumizi ya mtandao wametoa tamko la kuliomba Bunge lisipitishe Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao kuwa sheria, kwa kuwa unaingilia uhuru wa mawasiliano kwa wananchi.
Muswada huo unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki.
Wadau hao, muswada huo haukuwekwa wazi hadi tarehe 29 Machi na ratiba inaonesha muswada huo utapitishwa chini ya hati ya dharura tarehe 31 Machi, hivyo wananchi hawajapata nafasi ya kupitia kwa kina na kutoa maoni yao kuhusu muswada huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na wadau hao, iliyowakilisha wananchi wanaotumia mitandao muswada huo usipitishwe ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi kushiriki kikamilifu katika kuandika sheria hiyo muhimu.
“Sisi wadau tunaowakilisha wananchi wanaotumia mtandao tunaomba Bunge lisipitishe Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 kuwa sheria,” ilisema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Shirika la Sikika, Erinei Kiria.
Wadau hao walisema kuwa kutokana na umuhimu wa Muswada huo unaolenga kudhibiti uhalifu wa mitandao, lakini kwa namna ulivyo unaingilia uhuru wa mawasiliano.
“Muswada huu usipitishwe ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi kushiriki kikamilifu katika kuandika sheria hii muhimu,”ilisema taarifa hiyo .
Hata hivyo Muswada huo unalenga na kuhusisha kudhibiti mawasiliano ya wananchi wenyewe kwa wenyewe suala ambalo linaweza kupingana na katiba ya nchi sheria zilizopo na haki za binadamu za umoja wa mataifa.
Wiki iliyopita Bunge lilipitisha sheria ya Takwimu ambao unawabana wanahabari watakaoandika takwimu ambazo hazijaruhusiwa kutolewa na serikali wako hatarini kulipishwa faini ya Sh milioni 10 au kifungo kifungo kisichopungua mwaka miwili jela.
Mapendekezo ya adhabu hizo yako katika Muswada wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2013, ambayo ni miongoni mwa miswada miwili inayowasilishwa ndani ya Bunge.
Kwa mujibu wa ibara ya 20(1) ya sheria hiyo, muswada unataja taasisi tatu ambazo ndizo kisheria zitakuwa zikiruhusiwa kutoa au kuchapisha takwimu rasmi na si vinginevyo. Taasisi hizo ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Taasisi za Serikali na Wakala wa Serikali.

Kwa lugha rahisi, muswada unazuia waandishi na vyombo vyao kuacha kuandika habari za takwimu ambazo hazijatolewa rasmi na adhabu zake zinaanzia kifungo kisichopungua mwaka mmoja na faini ya kuanzia shilingi milioni tano na kuendelea.
“Mtu yeyote, kwa kujifanya anatimiza majukumu yake, iwapo anapata au anaomba kupatiwa taarifa ambayo haijaidhinishwa kuipata na kuichapisha au kuisambaza atakuwa amefanya kosa ambalo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi 12 au fani isiyopungua shilingi milioni mbili au vyote kwa pamoja,” inasema ibara ya 37 (d) cha muswada huo.
Muswada huo unaainisha wazi kwamba takwimu rasmi ni zile ambazo zimetolewa na kuidhinishwa na taasisi zilizoelezwa kwenye ibara hiyo ya 20 na ndizo pekee zinazoweza kutumika kama ushahidi kwenye kesi.

No comments :

Post a Comment