dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 25, 2015

WAZANZIBARI WAJA JUU: KAMA SIO MAKONGORO, BASI SAFARI HII NI MZANZIBARI !

Makongoro - The ony saviour of Tanganyika from "wizi, rushwa, tamaa, ujangiri wa rasilimali ya nchi hii na ufichaji wa pesa za kigeni huko Uswiss”!

Image result for lowassa
``Kumchaguwa tena mtu alietemwa ni sawa na kula matapishi. Sidhani kama Watanzania wapo tayari kula matapishi yao``.

Baada ya  mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa  kutamka hadharani kuwa sasa “ameshawishika” na kuweka bayana kuwa atachukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM),  Blog la Zanzibar Ni Kwetu lilitabiri hapo hapo kuwa atashinda katika uchaguzi wa October  na atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Rais Kikwete kuachia ngazi. 

Tokea tufanye utabiri huo, tumekuwa tukijuta, kwani simu zetu hazijasimama kulia mpaka hii leo na lines nyengine za ofisini kwetu imebidi ziwe dis-abled temporarily, kutokana na vilio vya Wazanzibari waliokerwa na utabiri wetu huo.

Wengi katika hao wanaotupigia simu wanatamka waziwazi kuwa wataweza kumuunga mkono kwa mikono yote miwili Makongoro Nyerere kama atachaguliwa na CCM kugombea urais, lakini hawatokuwa tayari kumuunga mkono mgombea mwengine yoyote yule kutoka Bara kama Makongoro atakataa kugombea katika mwaka huu wa 2015, kwasababu safari hii ni zamu yao Wazanzibari kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakijulishwa na Blog hili kuwa hakuna kipengele chochote katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kinachoelezea kuwa urais wa nchi utakuwa wa kupokezana baina ya Bara na Visiwani, Wazanzibari hao waliojaa hamasa walieleza kuwa…“Lazima tuuseme ukweli. Huu ni Muungano wa nchi mbili ambazo zilikuwa huru na zilikuwa na bendera zao wenyewe kwenye Umoja wa Mataifa. Haiwezekani Rais awe anatoka upande mmoja tu, kama vile upande mwengine hauna watu wanaofaa. Zaidi, hao wa upande wapili mara nyingi wanaongoza katika wizi, rushwa, tamaa, ujangiri wa rasilimali ya nchi hii na ufichaji wa pesa za kigeni huko Uswiss”.

Alivyoulizwa kwenye simu  mmoja wao kuwa kama wanao msimamo huo sasa kwanini wasipendekeze hivyo katika Katiba mpya? Alijibu kwa hamaki huku akiigongagonga simu yake na kuifanya isisikike vizuri kuwa…” Hivyo ndivyo tulivyopendekeza, lakini  maoni yetu yalitupiliwa mbali”.

Mara mwananchi mwengine aliekuwa kwenye simu nyengine akaendelea kujibu hata bila ya kuulizwa yeye suala hilo. ”Mlisikia na mliona wenyewe yaliomkuta mzee wetu. Mzee wa watu katia ombi letu la serikali 3 kwenye Rasimu na bahashishi yake ilikuwa kupigwa kiti cha kichwa. Je, kama  angelitia kwenye Rasimu kuwa wananchi wanataka urais uwe wakupokezana hivyo angeliishi mpaka leo?”, akamalizia mwananchi huyo na simu akaikata hapo hapo kwa hamaki.

Blog hili liliwauliza wapiga simu wengine, kwanini watamuunga mkono Makongoro Nyerere na hawatofanya hivyo kwa mwengine yoyote yule kutoka Bara, wakati Makongoro nae anatoka Bara pia?

”Huwezi kumlinganisha Makongoro na hao wengine wanaolilia kuiongoza nchi hii. Wote hao ni watumikia tumbo tu na hakuna msafi hata mmoja. Hao wengine wote washakuwa viongozi huko nyuma na wengine ni viongozi mpaka sasa, la kujiuliza ni kuwa wamefanya nini jema kwa nchi hii zaidi ya ufisadi nazi na wizi tu?. Zaidi, wengine  Nyerere alikwisha sema kuwa hawafai, kwani wanasifa ya kujilimbikizia mimali tu”, alimalizia kwenye simu mwananchi huyo.

“Tutamuunga mkono Makongoro kwasababu ni mtoto wa mfanyakazi na mkulima na sio bepari. Tunajua akipata yeye urais basi itakuwa tumeupata sisi sote wanyonge wa nchi hii.  Ule ujinga na upuuzi wa mtu kukamatwa na Dollar zaidi ya milioni moja na baadae kueleza kuwa hizo ni vijisenti tu, au mtu kutoa milioni 10 za wizi kutoka benki na baadae kusema kuwa hizo ni pesa za mboga tu, au watu kuhongana bilioni 330 wakati watoto wetu bado wanakaa chini mashuleni bila ya madawati - ujinga na upuuzi kama huo utakuwa umekwisha hapa nchini chini ya Makongoro”.

“Wewe tayari unao ng’ombe 1,000 kwenye zizi lako, sasa kwanini hujishughulishi na kuchunga hao ng’ombe wako na unataka kutuchunga sisi?”, aliuliza mwananchi mwengine kwenye simu.

“With 1000 heads of cattle, unknown number of buildings for rent and hotels,  you are a bourgeois capitalist, too rich to lead this nation of poor peasants and workers. Bepari kama wewe huwezi kutuongoza sisi walalahoi - wakwezi na wakulima. We need someone with a proven anti-rushwa record na sio mtu alietemwa na awamu moja na sasa agombee urais awamu nyengine. Kumchaguwa tena mtu alietemwa ni sawa na kula matapishi. Sidhani kama Watanzania wapo tayari kula matapishi yao”, aliendelea mwananchi huyo huku akichanganya ung’weng’we na kiswahili, kama vile kashuka leo kutoka UK.

Ukiachilia mbali vilio vya Wazanzibari, ishara zote zinaonesha kuwa Lowassa ndie atakae kuwa chaguo la CCM na ndie atakae kuwa Rais wa Jamhuri. Kama ni hivyo tunadhania kuwa atakuwa Rais wa mwanzo wa Jamhuri ambae atachaguliwa kutoka upande mmoja tu wa Muungano. Definitely, that would not make sense to any sensible person – even to Lowassa himself. Lakini, kama wanavyoeleza walimwengu, mwenye nguvu mpishe. Bwana Lowassa tutampisha Ikulu, lakini bila ya kura zetu!

No comments :

Post a Comment