dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 1, 2015

DUUUUUUUU...................HAYA MAELEZO YANATISHA KUHUSU ABDALLAH MZEE HOSPITAL (PEMBA)!!!!

Abdallah Mzee Hospital
Written by Ashakh (Kiongozi) 
Jengo la Hospital ya Abdalla Mzee. Jengo hili ambalo


. Dr Shein yu Uingireza
. Maalim Seif yu India


Kwa muda wa siku mbili nilikuwa nakesha kwenye jengo hili la Hospital ya Abdalla Mzee hapo Mkoani kufuatia ndugu yangu kufanyiwa operation. Hii ni mara ya mwanzo kuhudumia mgonjwa anapolazwa katika hospital zetu za Zanzibar.

Kama vile nilikuwa siamini ninapoambiwa kwamba Hospital zetu zinalala wagonjwa wawili kitanda kimoja, au wengine wanalala chini. Au hakuna hata kikombe cha chai kinachotolewa kwa wagonjwa wanaolazwa. Kubwa zaidi na huduma za matibabu zinazotolewa. Hivi kusikia mtu anafanyiwa upasuaji au kushonwa bila ya sindano ya ganzi.

Abdalla Mzee Hospital ndio hospital Kubwa hapa Pemba. Sasa hivi iko katika hatua za ujenzi wa majengo mapya eneo lilelile ingawa limetanuliwa zaidi. Tofauti na ilivyozoeleka kusikia neno “Karume”, bado hospital hii inatumia jina la Abdalla Mzee. Sihasha itakapokamilika ikabadilishwa jina na kuwa “Dr Ali Mohmed Shein”.

Hali ya afya za watu wetu ni mbaya sana. Jamani mengi nimeona nilipolala hapo.

Picha hizo hapo juu zinajionyesha, huo ni uliokuwa ukumbi wa mikutano wa Umoja ni nguvu mali ya CCM Wilaya ya Mkoano sasa ndio umefanywa kuwa wodi ya wazazi pia kwa wagonjwa wengine waliofanyiwa operation. Ndani kumekatwa petition kwa hardboard. Kuna chumba kimoja cha operation kimetiwa airconditon, chumba kimoja cha staff ndio wagonjwa wanaangaliwa, chumba kimoja cha kuzalishia na kimoja cha kulazwa.

Chumba cha kulazwa wagonjwa kuna vitanda vichache sana kiasi wagonjwa wanalala wawili wawili. Hakuna hata fan moja kwenye chumba hiki, fan lipo kwenye chumba cha kuzalishia na cha staff. Mbu wa hapo ni wakubwa sana kwa vile wanapata lishe ya kutosha.

Huduma ya umeme pia ni ya kusuasua, generator lipo halifanyi kazi. Juzi kulikuwa na kazi ya ku install solar power. Maji yapo ya kutosha kwani kuna tank 3, ya lita 10,000, lita 5,000 na lita 1,000.

Sikuona hata mara moja kigari cha vyakula kupitisha kutoa huduma kwa wagonjwa. Si wakati wa asubuhi, kutolewa uji, mchana kutolewa pilau wala usiku japo kipande cha embe. Nilipata taarifa kuna bibi mmoja mwenye imani yake huja siku vyengine na chupa za uji kugaiya wagonjwa. Nilipouliza hali yake kimaisha, nikaambiwa si mtu mwenye uwezo isipikuwa ni mtu na imani yake.

Wako jumla ya madaktari wawi; mmoja Mchina na mmoja Dr Idriss kutoka Kangani.


No comments :

Post a Comment