dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 28, 2015

CCM wanazika wafu wao, Chadema wanazuiwa

Joster Mwangulumbi , Mwananchi.
Hii ni aibu ya kujitakia kwa Serikali. Madaktari, manesi, mabwana na mabibi afya hufundisha kwamba kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na bakteria aitwaye “Vibrio cholera” na ni ugonjwa unaosambazwa kupitia kwenye kinyesi kutoka kwa wagonjwa wenye kipindupindu.
Lakini Serikali hiyo hiyo kupitia Jeshi la Polisi inasema kipindupindu kinaenezwa na vyama vya upinzani.
Wataalamu wa afya hufundisha kuwa mahali ambako hakuna usafi wa kutosha, hakuna maji ya mfereji au mabomba ya kupitisha maji machafu au maji machafu yasiyofunikwa, au maji ya kunywa yasiyofunikwa huchangia katika kusababisha mkurupuko wa kipindupindu. Lakini Polisi wanasema mkusanyiko wa wafuasi wa Chadema husambaza kipindupindu.
Madaktari husema dalili za ugonjwa huo ni kuharisha haja iliyo majimaji, mwili kushindwa kutumia maji na chakula hivyo basi kumfanya mgonjwa kudhoofika haraka kwa sababu ya kukosa maji mwilini, kuhisi kiu kingi na uchovu mwingi, na hushindwa kutulia, na ngozi ya nje na ndani kunyauka na macho kuingia ndani na kupata kichefuchefu na kiharusi kisicho cha kawaida.
Polisi wanasema dalili ni pale wanapojiandaa kuuaga mwili wa mpendwa wao. Kuepuka kipindupindu jamii hushauriwa wakati wote kunawa mikono kwa sababu kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe; kunywa maji yaliyochemshwa, kufunika chakula, kuhakikisha nzi hawatui kwenye chakula, kutumia vyoo, kuchemsha vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa. Polisi wanasema ili kuepuka ugonjwa huo, wafuasi wa Chadema na viongozi wao tu wawekewe karantini wasishiriki mazishi ya kiongozi mwenzao.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo amefariki dunia. Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, waliomuua ni wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ghafla msiba huo umegeuka kuwa kipindupindu cha siasa.
Kwa siku tatu askari wa Polisi walizungusha utepe kuwazuia wanachama wa Chadema kufika kwenye ofisi zao mjini Mwanza kupanga maandalizi ya kuchukua mwili wa Mawazo kwenda kuzika. Pia, wakaweka doria katika hospitali ya Bugando kuwazuia ndugu, jamaa, marafiki, wafuasi na viongozi wa Chadema kuchukua mwili waweze kuuaga kama ilivyo ada kwa binadamu wengine na kuuzika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alipiga marufuku akidai kuwa wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na kuwapo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie amedai Mawazo si kiongozi wa kitaifa wala mkazi wa mjini Geita.

Kipindupindu na misiba
Kipindupindu kilizuka Dar es Salaam Agosti 15 na kusambaa nchi nzima. Hadi Septemba 30 kilikuwa ‘kimechinja’ watu 36 katika jiji la Dar es Salaam na mamia wengine kulazwa katika hospitali za jijiji hilo. Ilitokea misiba minne ambayo haikuzuiwa na Jeshi la Polisi.
Kipindupindu hakikutumiwa kama sababu ya kuzuia mkusanyiko wa kumuaga aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani Septemba 28 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Pia, Serikali haikutumia kipindupindu kuzuia umati wa watu uliokusanyika Oktoba 15 kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania, Dk Abdallah Kigoda aliyefariki nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Baada ya kuagwa katika Viwanja vya Karimjee ulisafirishwa kwenda kwao Handeni, Tanga kwa mazishi.
Vilevile, Serikali haikuzuia kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa Filikunjombe Oktoba 17 aliyefariki dunia kwa ajali ya helikopta katika pori la Selous. Wengine walioagwa siku hiyo nyumbwani kwake Kijichi ni ndugu zake Plasdus Ngabuma na Casablanca Haule.
Oktoba 15 alifariki dunia aliyekuwa Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Dk Emmanuel Makaidi. Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha National League for Democracy (NLD) kwenye hospitali ya Nyangao, Mtwara kwa presha na mwili uliagwa kwa heshima zote Oktoba 20, 2015 kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Kila siku kuna watu wanakufa ama kwa majanga au kwa maradhi yakiwamo ya kipindupindu majumbani au hospitalini nchi nzima na maisha yanasonga mbele. Kwa nini iwe nongwa kwa Mawazo? Iwapi haki ya msingi ya Mawazo kuagwa na marafiki zake? Tatizo si kipindupindu ila ni Polisi kutumiwa kucheza siasa.

Siasa msibani
Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kila vikitokea vifo vyenye utata vinavyohusu wafuasi wa Chadema, Polisi huwaongezea machungu kwa kuwapiga waombolezaji kwa mabomu ya kutoa machozi na kuwatia ndani kwa madai wanafanya fujo.
Mei 24, 2011 ulitokea mvutano kati ya Polisi na Chadema kuhusu kibali cha kuzika watu wanne kati ya watano waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mgodi wa North Mara, na haki ya kukusanyika kuomboleza.
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Tarime, John Henjewele alisema Serikali itagharimia mazishi ya watu hao waliouawa Mei 16, lakini kilichotokea ni Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara kuvamia hospitali ya wilaya na kisha kutwaa miili ya marehemu hao na kuitelekeza katika vijiji vyao.
Katika tukio hilo ambalo Polisi walidai mkusanyiko wa waombolezaji haukuwa halali, watu 12 wakiwamo wabunge wawili wa Chadema; Tundu Lissu na Ester Matiko pamoja na aliyekuwa kada maarufu Waitara Mwita walikamatwa.
Juni 18, 2013 Polisi waliwatawanya kwa mabomu wafuasi wa Chadema walipokusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki Juni 15, 2013 kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani jijini Arusha. Tundu Lissu, Said Arfi na watu wengine 60 walitiwa ndani kwa kile Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alidai kufanya mkusanyiko usio halali.
Agosti 12, 2015 msafara wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema chini ya mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ulizuiwa ulipokuwa unakwenda kwenye kuhudhuria msiba wa kada wa CCM Peter Kisumo, Usangi. Polisi walidai msafara wake ni mkubwa sana na eneo ni dogo.
Safari hii, bila sababu za msingi, Polisi wakaamua kuzuia kuagwa mwili wa Mawazo eti wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na kuwapo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Naye Mkuu wa wilaya ya Geita, Manzie Mangochie akajitokeza na kudai eti Mawazo si kiongozi wa kitaifa wala mkazi wa mjini Geita. Kweli?

Maswali mepesi
Je, Mawazo alikufa kwa kipindupindu? Je, kuna karantini iliyowekwa mkoani Mwanza? Je, hakuna watu wengine wanaofariki, kuagwa na kuzikwa na ndugu, jamaa na wanasiasa kama ilivyo kwa Mawazo? Tangu lini Polisi wakapewa kazi ya kuratibu vifo vyote na kuona uhalali wa kuzikwa na watu wengi?
Watu 17 wamekufa Mwanza lakini watu 36 walikufa Dar es Salaam wakati makada wa CCM Kombani, Kigoda, na Filikunjombe wanaagwa mbona hawakuzuiwa?
Tangu lini Mangochie amekuwa msemaji wa wafiwa nchini kwamba huyu anastahili kuzikwa na watu wengi au la? Nani amempa kazi Mangochie ya kuratibu vifo vya watu na mahali wanapostahili kuzikwa?
Hivi hakuna raia wa kawaida kabisa na wengine wakulima wa hali ya chini wenye marafiki au ndugu ambao ni viongozi wa kisiasa kitaifa au watu mashuhuri serikalini kama ilivyo kwa Mawazo?
Je, Serikali inatarajia nini kwa hatua ya kuwasukuma Chadema hadi kwenye ukuta wa mwisho wa uvumilivu?

No comments :

Post a Comment