dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 18, 2015

HATARI YA KUTIZAMA PICHA ZA NGONO NI KULIKO HATARI YA KULA DAWA ZA KULEVYA (DRUGS)!


You must read this article kama wewe ni shetani wa kutizama xxx picha/video!

Picha za ngono ni hatari kwa afya ya ubongo


By Clifford Majani, Mwananchi
Utandawazi na ongezeko la maarifa katika teknolojia ya vifaa ya mawasiliano ya kidijitali, umesababisha kusambaa picha na video za ngono.
Picha na video hizo kwa sasa zinapatikana katika machapisho ya magazeti, kanda za video, redio simu za mkononi na kwenye kompyuta zenye mtandao wa intaneti kwa gharama nafuu na wakati mwingine zinapatikana bure.
Ripoti iliyotolewa na Asasi ya Internet Filter Review 2006, ilibainisha kuwa kila sekunde Dola za Marekani 3,076 hutumika kwa ajili ya kutazama picha za ngono mitandaoni.
Taarifa hiyo ilisema kuwa, zaidi ya watu 28,000 wanaotumia mtandao kila sekunde duniani hutazama picha za ngono na kila ndani ya dakika 39, video mpya inayoonyesha picha za ngono huzalishwa huko Marekani.
Hali hii huzifanya picha za ngono kuwa biashara namba tatu inayowaingizia baadhi ya matajiri duniani mabilioni ya dola ikiwa nyuma ya biashara ya dawa za kulevya na kamari.
Kutokana na ukweli kwamba picha hizi zinaangaliwa katika mazingira ya faragha, zimekuwa kivutio kwa watu wengi wanawake na wanaume hasa vijana.
Watu wengi huangalia picha hizi kwa lengo la kupata msisimko wa kingono, kujiliwaza au kujifunza mitindo mbalimbali ya kufanya tendo la kujamiiana wakiamini au kuaminishwa kuwa hazina madhara
Madhara kwa mtazamaji
Ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kuwa kuangalia picha hizi kwa muda mrefu, kunasababisha athari mbaya kwa afya ya kisaikolojia na kijamii, unaendelea kuongezeka.
Kwa kuwa picha za ngono ni kitu ambacho hakikuwapo siku za nyuma, kwa sasa ni kama zinafanyiwa majaribio katika jamii.
Takriban miaka 15 iliyopita tangu picha hizi zilipoanza kusambazwa kwa wingi, hakuna aliyekuwa anafahamu kinagaubaga kuhusu athari hasi za picha hizi kuhusiana na afya ya akili, utendaji wa ubongo, ufanisi wa tendo la ndoa na jinsi zinavyosababisha uraibu sawa na dawa za kulevya.
Kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, Dk Judith Gelernter Reisman ambaye ni profesa wa utafiti katika Chuo Kikuu cha Liberty Marekani, alizipatia picha hizi jina la “erototoxin,” akimaanisha kuwa zina uwezo wa kudhuru ubongo wa mtu anayezitazamani kwa muda mrefu.
Dk Reisman alibainisha kuwa vichocheo vya kemikali za mwili vinavyozalishwa kwa wingi na kusisimua neva kupita kiasi wakati wa kuangalia picha hizi, vina athari mbaya kwenye ubongo.
Kutokana na athari zake, watu wengi duniani kote wametekwa na mawazo ya ngono kuliko kitu chochote.
Katika utafiti uliofanywa na Terri Fisher pamoja na wenzake kutoka Chuo Kikuu cha Ohio (OSU) nchini Marekani na kuchapishwa mwaka 2012 katika jarida la utafiti wa masuala ya ngono (Journal of Sexual Research) toleo namba 49(1), ilibainika kuwa wanaume wengi siku hizi hufikiria tendo la ngono kwa wastani wa mara 19 kila siku, wakati wanawake wakifikiria ngono kwa wastani wa mara 10 kwa siku.
Katika utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2008 na kupewa jina la “Generation XXX,” watafiti pia walibaini kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi wengi vijana katika vyuo vikuu huko Marekani, wanaamini kuwa kuangalia picha za ngono ni jambo linalokubalika kimaadili. Utafiti huo pia ulibainisha kuwa wavulana tisa kati 10 na msichana mmoja kati ya watatu ni watazamaji wa picha za ngono.
Takwimu kadhaa kutoka nchini Uingereza zinabainisha kuwa hali si shwari kuhusiana na athari za picha za ngono.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha East London ulibainisha kuwa asilimia 97 ya wavulana na asilimia 80 ya wasichana kati ya miaka 16 na 20 wamewahi kuangalia picha za ngono. Ripoti nyingi pia zinaonyesha kuwa kwa kila vijana 25 nchini humo, mmoja ana uraibu wa ngono.

Utazamaji wa ngono Afrika
Ni vigumu kupata takwimu za utazamaji wa picha za ngono, tafiti kadhaa zinabainisha kuwa hali si shwari.
Kutokana na sheria kuzuia usambazaji wa picha za utupu, ni vigumu kupata takwimu za watu wanaoangalia picha za ngono mara kwa mara, lakini ukweli ni kwamba hali ni mbaya katika kipindi hiki ambacho watu wengi wanapata mtandao wa intaneti kupitia kompyuta na simu za mkononi.
Hali hii inalazimisha mashirika mengi kuweka utaratibu wa kitaalamu kudhibiti uangaliaji wa picha za ngono kwenye komputa zilizoko ofisini.
Mtu mwenye hali ya uraibu au ulevi wa ngono kila wakati anawaza kuhusu ngono kiasi kwamba anaweza hata kushindwa kutekeleza majukumu ya kiofisi na majukumu mengine ambayo ni muhimu kwa mafanikio ya mtu binafsi na maendeleo ya jamii kwa jumla.
Ulevi wa ngono mbali na kuathiri afya ya mhusika pamoja na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi, unaweza pia kuchochea vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii.

Athari kwenye ubongo
Matokeo ya utafiti uliofanywa na jopo la watafiti kutoka katika Chuo Kikuu cha Cambridge na kuchapishwa hivi karibuni katika jarida liitwalo Psychiatric Research, yanaonyesha kuwa ubongo wa mtu aliyezoea kuangalia picha za ngono hauridhishwi na kuona aina moja ya taswira inayohusu ngono.
Utafiti huo unaongeza kusema kwamba hali hii humfanya mtu mwenye mazoea haya kufanya jitihada za kutafuta taswira mpya kila mara, ili kutimiza matakwa na matamanio yaliyojengeka katika akili yake.
Utafiti mwingine ulioongozwa na Dk Valerie Voon wa Kitivo cha Magonjwa ya Akili katika Chuo Kikuu Cambridge, ilibainika kuwa athari za uraibu wa ngono kwenye ubongo, zinafanana na athari za dawa za kulevya hali ambayo inawafanya watu wenye uraibu wa ngono kushindwa kuachana na mazoea ya kuangalia picha za ngono.
Dk William Struthers, daktari bingwa wa mfumo wa fahamu na mwandishi wa kitabu kiitwacho ‘Wired for Intimacy: How Pornography Hijacks the Male Brain,’ naye anayaelezea mazoea ya kuangalia picha za ngono kuwa yanaathiri sehemu ya ubongo iitwayo ‘cingulate cortex’ ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia mtu kudumisha nguvu ya utashi na kufanya maamuzi mazuri ya kimaadili.
Wanasayansi wanabainisha kuwa wakati wa kusisimka kingono, kemikali aina ya dopamine huzalishwa na kuingia katika sehemu ya ubongo inayohusika na hisia pamoja na kujifunza mambo na hapo huzalisha hisia za raha.
Mhusika anapopata tena hisia za ngono, kemikali hiyo huingia tena katika ubongo na kuziambia seli za ubongo kukumbuka kile kilichomfurahisha mhusika katika tukio la nyuma wakati alipopata msisimko wa ngono.
Msisimuko wa kingono pia huzalisha vichocheo vya oxytocin na vasopressin.
Vichocheo hivi pia hufanya seli za ubongo ziwe na kumbukumbu ya muda mrefu kuhusu kitu kilichomfanya mhusika apate raha kupita kiasi. Wakati huo kichocheo cha norepinephrine pia huzalishwa na kuuambia ubongo ujiandae kwa tendo la ngono.
Hali hii inayohusisha wingi wa kemikali za mwili kuingia katika ubongo, ndiyo inayozalisha uraibu na athari za ubongo kwa watazamaji wa mara kwa mara wa picha za ngono.
Baadhi ya watafiti wanasema kwamba mbali na raha anayopata mtu anayeangalia picha za ngono baada ya kutimiza haja za ngono, pia mtu huyu hupata hisia za wasiwasi na kujilaumu kimaadili na akili yake haipendi watu wengine wajue kuwa ana tabia hiyo.
Mtaalam wetu wa magonjwa ya binadamu, Dk Shita Samwel anaunga mkono utafiti huu, anaeleza kuwa teknolojia zina faida lakini zinaweza pia kuwa na madhara yake. Kwa vijana ambao wako umri wa baleghe ndio walio katika hatari zaidi ya kupata ushawishi wa kujiingiza katika ngono zembe mapema na kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU na magonjwa ya zinaa. Picha hizo hapo baadaye ukubwani zinaweza kuwafanya kuhitaji kujiridhisha kihisia kwa kutazama tu badala ya kuhitaji tendo halisi.

1 comment :