dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 3, 2016

Balozi Norway atembelea ofisi za CUF Zanzibar

Balozi wa Norway, Hanne-Marie Kaarstad

By Hassan Ali, Mwananchi 
Zanzibar. Siku nne baada ya mabalozi wa nchi 17 kutoa tamko likimtaka Rais John Magufuli kuingilia kati mgogoro wa Zanzibar, balozi wa Norway, Hanne-Marie Kaarstad jana alitembelea ofisi za CUF, Vuga visiwani humo na kufanya mazungumzo na maofisa wa chama hicho.
Balozi huyo na ujumbe wake walifika katika ofisi hizo saa 8.30 mchana jana na kukutana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Mazrui na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu
Jussa alithibitisha kutembelewa na Balozi Kaarstad ambaye ni miongoni mwa mabalozi 16 wa nchi za Ulaya na Marekani waliotoa tamko hilo, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani yaliyozungumzwa.
“Ni kweli ametutembelea pamoja na ujumbe wake, lakini mazungumzo kati yetu yalikuwa ya ndani,” alisema Jussa.
Alisema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad hakuwapo katika kikao hicho, na kwamba wageni hao hawakusema kama wanataka kukutana naye.
Januari 29, mabalozi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya (EU), Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Uswisi, Uingereza na Marekani walitoa tamko la wito wa kuendelezwa kwa mazungumzo baina ya pande zote za mgogoro.
Wakati huohuo, Maalim Seif leo anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya matawi, majimbo na wilaya upande wa Unguja na kesho atafanya hivyo kisiwani Pemba.
Mjini Unguja, kikao hicho kitafanyika ukumbi wa Majid, Wilaya ya Magharibi ambako Maalim Seif, anatarajiwa kuweka bayana juu ya hali ya kisiasa na mikakati ya chama hicho.
“Huo ni mkutano wa kawaida, unajua hiki ni chama cha wananchi, mkutano unalenga kuwaelewesha hali iliyopo sasa na juhudi zinazoendelea kuhakikisha ushindi unabaki mikononi mwetu,” alisema mmoja wa watendaji wa CUF Zanzibar.
Mikutano hiyo inafanyika wakati chama hicho kikiwa kimeweka msimamo wa kutoshiriki uchaguzi wa marudio Machi 20, uliotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), baada ya ule wa Oktoba 25 kufutwa. 

No comments :

Post a Comment