dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 11, 2016

Kikwete: Nitatumia uzoefu wangu kuiendeleza UDSM.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha  Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, amesema atatumia uwezo na vipaji vyake  kuhakikisha chuo hicho  kinaendelea kuwa bora na kinatoa viongozi wa taifa. 
 
Dk Kikwete aliyasema hayo juzi mara baada ya kumaliza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo chuo hicho.
 
Miradi ambayo ameitembelea Dk. Kikwete ni pamoja na kituo cha mafunzo ya elimu, jengo la sayansi, eneo la maegesho na jengo la mihadhara la Yombo ambalo lina eneo la maktaba mpya.
 
Alisema changamoto ambazo zinakikabili chuo hicho nazo atazifanyia kazi kutokana na kuwa na uzoefu katika serikali kwa miaka mingi. 
 
Aliongeza kuwa atapitia taratibu kwa kuisoma taarifa iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Rwekeza Mukandara, kisha kuitolea majibu kipindi ambacho watakutana tena mwishoni mwa mwezi huu.
 
Dk. Kikwete alipongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuboresha miundombinu ambayo imekuwa kichocheo cha kuongezeka kwa  wanafunzi.
 
Pia alimshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumwamini na kumteua kwa kuwa mkuu wa chuo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment