dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 11, 2016

Mapato Hospitali ya Muhimbili yaongezeka kwa asilimia 60

By Herieth Makwetta, Mwananchi
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza mapato yake kwa asilimia 60, baada ya kuboresha usimamizi na kupunguza kero za wafanyakazi, huku ikitekeleza kwa asilimia 100 maagizo matatu ya Rais John Magufuli.
Maagizo hayo yalitolewa na Dk Magufuli siku nne baada ya kuapishwa alipotembelea hospitali hiyo, Novemba 9 mwaka jana yametekelezwa kutokana na kuhudumia wagonjwa wengi zaidi na kwa wakati.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya MNH katika siku 100 za Rais Magufuli madarakani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema hospitali hiyo imeongeza uzalishaji wenye tija pamoja na kiwango cha ukusanyaji wa mapato.
Alisema kwa Desemba pekee, walikusanya Sh3.3 bilioni kutoka wastani wa Sh2.7 bilioni ilizokuwa ikikusanya kwa kipindi cha miezi mitano iliyotangulia.
“Tumepiga hatua, kwani Januari mwaka huu tumeweza kukusanya kiasi cha Sh4.3 bilioni. Katika mipango yetu ya muda mfupi iliyopo sasa tumepanga kukusanya Sh6 bilioni ifikapo Julai mwaka huu,” alisema.
Profesa Museru alisema watekeleza maagizo ya Rais Magufuli kuhusu mashine za MRI na CT Scan ambazo sasa zinafanya kazi vizuri, wagonjwa hawalali chini na upatikanaji wa dawa ni mzuri
Alisema matengenezo ya mashine ya MRI yalifanyika kikamilifu na tangu ilipotengamaa imepima zaidi ya wagonjwa 2,200.
Mkurugenzi huyo alisema wagonjwa waliokuwa wanalala chini wamehamishiwa katika wodi zingine na ile waliyokuwa wanatumia inafanyiwa matengenezo yanayotarajiwa kukamilika wiki mbili kuanzia sasa.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa MNH, Gerald Jeremiah alisema ukusanyaji wa mapato umeiwezesha hospitali hiyo kulipa madeni iliyokuwa ikidaiwa na wafanyakazi na wazabuni.
“Wafanyakazi walikuwa wanadai Sh600 milioni na wameshalipwa tangu mwanzoni mwa Februari mwaka huu, kulikuwa na madeni ya wazabuni na wengine wanaoleta vifaa mbalimbali kiasi cha Sh5.7 bilioni nazo zimelipwa,” alisema.
Alisema hospitali ilikuwa na deni la Tanesco linalofikia Sh4.6 bilioni ambalo Serikali ilisaidia kulilipa na kwamba, kwa sasa ina deni la mkopo wa Bima ya Afya la Sh3.4 bilioni.     

No comments :

Post a Comment