dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 16, 2016

NAFAZI ZA KAZI BODI YA MAPATO ZANZIBAR (ZRB) MWISHO WA KUTUMA MAOMBI 22/4/2016

Image result for Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB)


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imeanzishwa chini ya Sheria Namba 7 ya mwaka 1996 ikiwa ni Taasisi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na vianzio vya ndani.
Katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali, ZRB imekusudia kujaza nafasi mbalimbali zikiwemo:
. AFISA HABARI NA MAHUSIANO DARAJA LA II NAFASI MBILI (2) KWA AFISI YA ZRB UNGUJA
SIFA ZA MUOMBAJI
• Awe Mzanzibari.
• Awe na shahada ya kwanza katika fani ya Uandishi wa habari, uhusiano (Public Relations) au Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kingereza na kiswahili kwa ufasaha.
• Awe mfuatiliaji mzuri na mwelewa wa taarifa na matukio mbalimbali ya Uchumi, Biashara na Kodi kupitia vyombo vya habari.
• Awe na uwezo wa kutumia kompyuta.
• Awe na umri usiozidi miaka thalathini na tano (35)
• Awe mbunifu na awe na uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa
KAZI ZAKE:
• Kujibu hoja mbalimbali kwa kupitia simu, emails za wateja wanaouliza masuala ya kodi.
• Kupokea malalamiko ya wateja na wadau wakodi yaliyowasilishwa kwa njia ya simu na email.
• Kukutana na walipakodi na wadau wengine kwa lengo na kuwasikiliza na kufuatilia shida zao.
• Kutoa maelekezo kwa walipakodi na wadau wengine kuhusiana na ujazaji wa ritani na fomu nyenginezo za ZRB.
• Kujumuisha malalamiko ya wateja na wadau wengine na kuandaa ripoti yake.
• Kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya habari kuhusiana na matukio mbalimbali.
• Kufuatilia na kujibu hoja mbalimbali zinazotolewa dhidi ya ZRB.
APPLICATION INSTRUCTIONS:
NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua ya maombi iambatanishwe na maelezo binafsi (CV) inayoonesha wadhamini wawili na namba zao za simu, namba ya simu ya muombaji,kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari, Vyeti vya kumalizia Masomo,cheti cha kuzaliwa na picha mbili.(2) za passport size zilizopigwa karibuni.
Maombi yote yawasilishwe makamo makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar kwa kutumia anuwani iliyopo hapa chini si zaidi tarehe 22/4/2016.
KAMISHNA,
BODI YA MAPATO ZANZIBAR
P.O.BOX 2072, MAZIZINI
ZANZIBAR.

No comments :

Post a Comment