dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 21, 2016

MOJA YA NDEGE MPYA ZA ATCL YAWASILI JIJINI DAR TAREHE 21 SEPTEMBER, 2016!

 Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo. 
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo. 


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo. 
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo

20 Septemba, 2016
Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

No comments :

Post a Comment