Kauli mbiu ya kongamano hilo ilikuwa ni 'MTU KWAO NDIO NGAO’ ilifuatana na ujumbe mzito wa mwaka huu ambao ulikuwa ni “Mtizamo mpya wa Kuimarisha Utalii wa Tanzania na uekezaji”.
Kongamano hilo lilifanyika kwa muda wa siku mbili kati ya tarehe 24 na 25 Augosti na lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, AlHajj Dr Ali Mohammed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ambae aliwakilishwa na Waziri wa Muungano Mhe Makamba, katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Makachori wa Zanzibar Ni Kwetu waliohudhuria kongamano hilo wameeleza kuwa inaelekea huenda kongamano la tano likafanyika mjini Chake Chake, Pemba, wakati lile la nne huenda likafanyika mjini Dodoma au Arusha. Kongamano la kwanza na la pili yote yalifanyika mjini Dar Es Salaam.
No comments :
Post a Comment