dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 29, 2017

Viwanja 10 kupigwa mnada kwa kutolipiwa kodi!

SERIKALI imewataka wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipia kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kunyang’anywa umiliki wa ardhi zao.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mboza Lwandiko, wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Mboza alisema wizara inakusudia kufanya mnada wa viwanja 10 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni ambavyo havijalipiwa kodi ya pango la ardhi mpaka Machi 24, mwaka huu.

“Usipolipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati, utanyang’anywa umiliki wa ardhi yako, kutokana na sheria ya Ardhi, Na. 4 ya mwaka 1999, katika kifungu cha 49 na 51,” alisema Mboza.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Kodi katika wizara hiyo, Denis Masami alitoa ufafanuzi wa utaratibu unaotumika kuwasiliana na wamiliki wa ardhi walioshindwa kulipa kodi kwa wakati na kusema kwamba wadaiwa wanapewa hati ya madai na kupewa muda wa kukamilisha madeni yao.

Muda wa kukamilisha malipo ukipita, amri ya mahakama ya kukamata mali hufuata, ambapo mmiliki wa ardhi atatakiwa kuikomboa ardhi yake kwa kulipa deni mara moja, akishindwa mahakama hutoa amri ya kuuza mali.

Mahakama imetoa amri ya kwanza Januari 27, mwaka huu ya kukamata mali kwa wadaiwa sugu na Januari 24, mwaka huu mahakama ilitoa kibali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuuza kwa mnada wa hadhara viwanja ambavyo havijalipiwa kodi ya pango la ardhi.

“Tarehe 20 Machi, 2017 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilitoa tangazo la mnada wa hadhara wa kuuza viwanja ambavyo havijalipiwa kodi ya ardhi unaotarajiwa kufanyika Machi 26, 2017,” alieleza Masami.

Aliongeza kwamba wizara imeandaa orodha ya wadaiwa sugu, mpaka sasa katika orodha hiyo baadhi ya viwanja vimelipiwa sehemu ya kodi inayodaiwa baada ya wamiliki kuomba kukamilisha sehemu iliyobaki kabla ya kumalizika kwa muhula huo.

Alitoa rai kwa Watanzania wanaomiliki ardhi kujifunza utamaduni wa kulipia kodi pasipo shurti. Kodi ya ardhi hulipiwa kila ifikapo Julai mosi ya kila mwaka katika Manispaa au Halmashauri husika na katika Ofisi za Malipo ya Kodi-Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment