dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 15, 2017

ZANZIBAR: PBZ yatangaza faida ya 15.7bn/-

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Juma Ameir Hafidh

BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ), imesema imepata faida ya shilingi bilioni 15.7 kabla ya kodi katika kipindi cha miezi tisa kutoka Januari hadi Septemba mwaka huu.
Faida hiyo ni kubwa ikilinganishwa na shilingi bilioni 12.8 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2016.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mperani, Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Juma Ameir Hafidh, alisema faida hiyo ni ongezeko la shilingi bilioni 2.9 sawa na asilimia 22.7.
Alisema faida iliyopatikana, imevuka lengo la ukusanyaji faida katika kipindi hiki kwa asilimia 14.4 ambapo matarajio, ilikuwa ni kupata faida ya shilingi bilioni 13.7.
“Kipimo mashuhuri cha faida kwa kulinganisha na mali za benki (ROA) kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2017, kilikuwa ni silimia 2.66 ni rikodi iliyo bora, hasa kwa kuzingatia kuwa ni kipimo kilichokuwa juu ya wastani kwa mabenki yote Tanzania,” alifahamisha.
Kuhusu kuongezeka la wateja, alisema PBZ imeongeza wateja 14,359 kutoka 171,852 mwezi Disemba hadi kufikia 186,211 mwishoni mwa robo ya tatu ya 2017.
Hali hiyo imepelekea kukua kwa amana za wateja kufikia shilingi bilioni 479.9 hadi Septemba 2017, ikilinganishwa na shilingi bilioni 423.4 zilizokusanywa hadi kufikia mwishoni mwa Disemba 2016, ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 56.5 sawa na asilimia 13.
Alifahamisha, mizani za benki nazo pia zimeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 576.17 kutoka shilingi 503.6 bilioni mwezi Disemba 2016, ongezeko ambalo la shilingi bilioni 72.6 sawa na asilimia 14.4 na ni zaidi ya wastani wa ukuaji wa mizania za mabenki yote Tanzania.
Pamoja na ukuaji huo na imani zinazotokana na wateja wa PBZ kwa kuweka amana zao, alisema benki imeongeza imani kwa wateja wao wakopaji licha ya changamoto mbali mbali zinazowakabili.
“Mpaka kufikia mwisho wa Septemba 2017, benki imetoa mikopo ya shilingi bilioni 332.6 ikilinganishwa na mikopo ya shilingi bilioni 316.5 zilizotolewa hadi kufikia mwishoni mwa Juni 2017,” alisema.
“Hapa kuna ongezeko la shilingi bilioni 15.5 sawa na asilimia tano, napenda kuwafahamisha ndugu zangu wananchi kuwa, sehemu kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyakazi wa taasisi za umma na serikali pamoja na wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa,” aliongeza.
Alieleza faida na mafanikio hayo waliyoyapata, yametokana na imani kubwa kutoka kwa wananchi kwa kuweka amana zao, vile vile kutumia huduma mbali mbali za PBZ, kama kuweka amana zao, huduma za mikopo, kusafirisha fedha nje ya nchi, kutumia huduma za Western Union, kulipia kodi kwenye matawi ya PBZ pamoja na huduma nyengine.

Hivyo amewaomba wananchi kutumia fursa nzuri na za haraka zinazotolewa na PBZ ili waweze kupata mafaniko pamoja na benki kupiga hatua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd PBZ Juma Ameir Hafidh akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar mafanikio yaliopatikana kwa PBZ Kwa Muhula wa tatu kwa mwaka 2017, mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya PBZ mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi akisoma Taarifa ya Mafanikio ya Benki kwa muhula wa Tatu wa mwaka 2017, na kutoa m,aelezo faida iliopatikana kupitia huduma za kibenki kwa Wananchi wanaopata huduma hizo kupitia PBZ kwa Zanzibar na Tanzania Bara na kusisitiza zaidi ya Wafanyakazi wa SMZ na SMT wamechukua mikopo kupitia PBZ, mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya PBZ katika jengo la Shirika la Bima Mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji Juma Ameir Hafidh akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa akitowa Taarifa ya mafanikio ya PBZ katika ukumbi wa Makao Makuu ya PBZ yalioko jengo la Shirika la Bima Mpirani Zanzibar. 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidh akitowa taarifa kwa waandishi wa habari Zanzibar.



No comments :

Post a Comment