dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 29, 2012

WAZANZIBARI WAILAANI ZANZIBAR!!!

WAZANZIBARI WAISHIO TORONTO WAILAANI ZANZIBAR !!!

  • Inayolaaniwa ni Nightclub ya Toronto yenye jina la ZANZIBAR!
  • Mayor Rob Ford wa Toronto kupelekewa petition
“Wazanzibari wanaoishi katika mji wa Toronto, Canada, pamoja na vitongoji vyake, kila siku wanakasirishwa sana na kuilaani ZANZIBAR”. Hayo yalisemwa leo na Katibu wa ZACADIA. ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) ni Jumuia ya Wazanzibari wanaoishi nje ya Zanzibar katika nchi ya Canada na ni chombo muhimu kinachowaunganisha Wazanzibari wanaoishi ughaibuni Canada.

ZANZIBAR inayolaaniwa ni ile klabu ya Toronto yenye jina hilo. Kwa Toronto neno ZANZIBAR ni jina la NIGHTCLUB moja maarufu sana kwa mambo ya ufuska, ukahaba na ngono ambayo ipo katikati ya huu mji kwenye mtaa wa Yonge (# 359) unayoigawa Toronto pande mbili - Mashariki na Magharibi. Zanzibar Nightclub inamambo machafu tele ndani yake na imekuwa ikifanya biashara hii kwa muda mrefu sana - tokea 1960 ilipofunguliwa.


A strip club in the heart of Toronto named after the beautiful Islands of ZANZIBAR 
- this deeply enrages Zanzibaris living in Toronto!

Kusudio la Wazanzibari hawa ni kupeleka petition huko City Hall kwa Mayor wa Jiji la Toronto Bw. Rob Ford ili hii klabu ya mambo ya ufuska isipate licence chini ya jina la nchi yao tukufu na takatifu ya Zanzibar.

“Sio kama mambo haya hakuna huko kwetu Zanzibar hasa kwa siku hizi, lakini linalotusikitisha sisi ni kuwa, the only thing Torontonians know about our country (Zanzibar) is this nightclub. To them, the word ZANZIBAR is synonymous with prostitution, sex and alcohol. Kama hii klabu ingelikuwa huko Dar-Es-Salaam au Nairobi basi ingelikuwa sio kitu, kwani Zanzibar inajulikana kote huko kuwa ni nchi ya ki-Mapinduzi, lakini kwa hapa Toronto tunajulikana kama ni nchi ya upuuzi kutokana na sura mbaya hii klabu inayotupa”, alielezea Mzanzibari mmoja kwa masikitiko makubwa huku akitikisa kichwa chake kwa uchungu.



Dada huyo anaelekea kazini kwenye Zanzibar Club na mshashi kwa mbali anamperemba!

Above: Night photos of ZANZIBAR - Toronto's wildest strip club.  ZANZIBAR features dozens and dozens of  hot girls prostituting openly, live nude dancing, lap dancing, private VIP rooms, bottle service, all day and all night long. No cover, admission or minimum charge is required of  prostitutes going in for hunting safaris.

“Muulize mtu yoyote mitaani hapa Toronto nini ZANZIBAR na atakuambia kuwa hapo ndipo kilipo kitovu cha umalaya katika mji wa Toronto”, aliendelea kuelezea Mzanzibari mwengine.

Zanzibar Nightclub inamilikiwa na Mcanada mmoja anaeitwa Allen Cooper. Jitihada za kumpata babu yake (retiree) na kumuuliza alilipata wapi jina hilo hazikufanikiwa. Allen mwenyewe hajui na wala hajui Zanzibar maana yake ni nini!

Walipoulizwa baadhi ya wenyeji wa mjini Toronto ambao kila weekend wanaitembelea klabu hii juu ya nia ya Wazanzibari waishio Toronto kutaka jina la klabu hii libadilishwe, walijibu…"We have no problem with that at all. Let them give us another exotic name as sexy as the Zanzibar name is", and went on to add that, "What Zanzibaris do not understand is that, their beautiful Islands are being advertised from Toronto to the whole world at gratis.”

Asked about some bizarre sex activities being promoted at the Zanzibar place, some replied by saying that …"Nothing unheard of in sexual relationship is being promoted at the place. The best way to advertise today is through sex. A number of people who have visited the club ended up visiting Zanzibar Islands in real times. Thus, Zanzibaris do need to realize that as far as tourism is concerned, the Club works to the economic advantage of their country and therefore they should stop lamenting".

"The name Zanzibar boasts in spades a true African culture - a culture of mixed races, a friendly religious people, a humble nation and above all a natural beauty that is incomparable to any part of the world. As they say, if you don't live in Zanzibar, you are then just camping out there - wherever you are! Why would one associate such a good name of a beautiful country of a beautiful people with a strip club?", queried a young Zanzibari sympathetic to his countrymen who are petitioning to the Mayor against the Zanzibar Nightclub.

"Kuna wale watakaouliza eti tulikuwa wapi Wazanzibari tokea 1960 ilipoanzishwa klabu hii? Ukweli ni kuwa Wazanzibari tumeanza kuja Canada baada ya 1995 na kwahivyo yaliokuwa yakitendeka hapa Canada kabla ya hapo hatukuwa tukiyajua", alielezea kijana mmoja wa ki-zanzibari.

Alipopigiwa simu Katibu wa Jumuiya ya Zacadia na kuulizwa juu ya ukweli wa hatua wanazotaka kuzichukua dhidi ya hii klabu, alisema…" Nia tunayo, sababu tunayo, hivi sasa tunangojea wakati muafaka tu ili tui-lodge petition yetu kwa Mayor Rob Ford, huko City Hall".

 Toronto City Hall where Zanzibaris will soon lodge their petition to the Mayor

 Downtown Toronto where most of the Nightclubs are located

Toronto City with the CN Tower landmark towering the horizon

Compiled for ZNK by Khalid Abeid in Zanzibar and Said Bakar and Said Issa in Toronto, Canada.
Photos: Courtesy of Google

No comments :

Post a Comment