dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 31, 2018

Mtanzania auwawa na mpenzi wake Uingereza!


Image result for innalillahi wa inna ilahi
Image result for innalillahi wa inna ilahi
 Leyla akiwa na anaedaiwa kuwa mpenzi wake.
MWANAMAMA Leyla Mtumwa (36) mkazi wa Arusha ameuawa jijini London nchini Uingereza kwa kuchomwa visu na mwanaume mwenye umri wa miaka 38 (jina halijatajwa) anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake baada ya kutoka disco usiku wa kuamkia jana Machi 30, wote hawa ni Raia wa Tanzania.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kamkia jana Machi 30, 2018, katika nyumba wanayoishi Watanzania hao iliyopo eneo la Haringey, Kirkstall Avenue, N17  jijini London, baada ya kuzuka ugomvi baina yao ikiwa ni muda mfupi baada Leyla kurejea nyumbani akitokea disco la usiku alikokuwa amekwenda na marafiki zake.

Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa, alirudi kutoka disco akiwa na rafiki yake wamelewa na kuingia ndani, ambapo alimkuta mpenzi wake  ambaye alianza kufoka na kutukana jambo lililoibua mzozo mkali baina yao.

Baada ya mzozo huo kuwa mkubwa rafiki aliondoka na ndipo jamaa huyo alianza kumshushia kipigo kisha kumchoma visu mbele ya mtoto wake wa miaka 12, ambaye Leyla alizaa na mumewe wa kwanza anayedaiwa kuwa ni raia wa Nigeria.

Ikiwa ni majira ya saa 1:00 asubuhi, hali ya Leyla ilikuwa mbaya, kijana huyo alipiga simu katika kitengo maalum cha polisi cha makosa ya jinai (Met’s Homicide and Major Crime Command), kuwajulisha tukio hilo.

Kwa mujibu wa Met’s Homicide and Major Crime Command, baada ya polisi kuwasili walimkuta Leyla akiugulia majeraha ya visu huku akilia maumivu makali aliyokuwa akiyapata, walimchukua kwa Ambulance na kumpeleka hospitali.

Licha ya jitihada za polisi kuwahi, lakini Leyla aliaga dunia majira ya saa 2:11 asubuhi kwa saa za London. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakimshikilia mwanaume huyo wa Leyla kama mtuhumiwa namba moja wa tukio hilo.





No comments :

Post a Comment